24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ummy ashangaa ukimya wa wazazi watoto wakilawitiwa

Nora Damian, Dar es Salaam

Watu 116,899 wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2018 wakiwamo watoto na watu wazima.

Kati yao 78,400 ni watu wazima na 38,499 ni watoto ambao walipata huduma kupitia madawati 420 ya jinsia na watoto katika vituo mbalimbali vya polisi nchini.

Akizungumza leo Alhamisi Februari 13, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema amekuwa akipata kesi nyingi huku nyingine zikiwa katika hali mbaya.

Waziri Ummy alikuwa akizungumza wakati wa mkutano na waasisi wa Jumuiya ya Wanawake katika Nchi Huru za Afrika (PAWO) Tawi la Tanzania, uliokuwa na lengo la kupitia na kutoa maoni kwenye rasimu ya sera ya wanawake na jinsia ambayo inafanyiwa mapitio hivi sasa.

“Inakuwaje mtoto analawitiwa mara ya kwanza, ya pili, ya tatu… mama na baba mko nyumbani je, tunakosea wapi? Napata kesi nyingi, mtu anakuja tayari mtoto ameshaharibiwa.

“Kuhasiwa haitatusaidia, miaka 30 jela bado ni adhabu kubwa sana lakini watu hawaachi. Ni jukumu letu kwa pamoja kuzuia vitendo vya ulawiti na ubakaji hivyo kila mmoja atimize wajibu wake,” amesema Ummy.

Hata hivyo, amesema madawati ya jinsia yameongeza mwamko wa wananchi katika kujiamini na kutoa taarifa za ukatili pale unapotokea kwenye maeneo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles