25.5 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

CRDB yadhamini tamasha Sauti za Busara

Jeremia Ernest, Zanzibar

Tamasha la Sauti za Busara msimu wa 17 limezinduliwa leo visiwani Zanzibar katika eneo la kihistoria Ngome Kongwe likiwa na wadhamini mbalimbali ikiwemo benki ya CRDB.

Benki hiyo imetoa Sh milioni 20 kwa ajili ya kuchangia tamasha hilo ambalo limekua likichangia uchumi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza na Mtanzania Digital, mwakilishi wa CRDB Mbwana Ahmed, amesema wametoa udhamini huo katika tamasha hilo ili kuibua vipaji vya vijana, kutangaza vivutio na kuongeza uzalishaji.

“Tamasha la Sauti za Busara lina mchango mkubwa katika tasnia ya muziki linainua vipaji vya wasanii ambao bado ni vijana lakini pia linatangaza vivutio vyetu na kukuza pato la taifa, hii ndiyo sababu mwaka huu CRDB tumeamua kuwa miongoni mwa wadhamini wa kufanikisha tamasha hili,” amesema Ahmed.

Pamoja na mambo mengine, amesema CRDB imeandaa shindano kwa wateja wake kupitia mitandao yao ya kijamii ambapo washindi wanne kutoka Dar es Salaam pamoja na wapenzi wao watakuja kuhudhuria tamasha hilo.

Tamasha hilo limezinduliwa kwa maandamano kutokea Mapinduzi Square hadi Ngome Kongwe kwa gwaride la ‘Carnival’ ambalo limekua moja ya kivutio kikubwa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles