25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Mapambano ya Serikali kutokomeza saratani nchini

Sa AVELINE KITOMARY

ARATANI ni neno lililotolewa kwa kundi la magonjwa yanayoshabihiana. Kuna aina tofauti zaidi ya 100 ya magonjwa yanayoitwa saratani. Katika aina zote hizi, baadhi ya seli za mwili huanza kujigawa bila kusimama na kuenea kwenye maeneo ya karibu ya mwili.

Saratani inaweza kuanza kwenye sehemu yoyote ya mwili. Kwa kawaida, seli za mwili hujigawa na kuzalisha seli mpya kulingana na mahitaji ya mwili, seli za zamani zikiharibika au kuzeeka, seli mpya huchukua nafasi ya seli hizo.

Saratani inapotokea, mpangilio huu huvurugika. Kadiri uvurugikaji huu unavyozidi, seli za zamani zinaendelea kuishi badala ya kufa na seli mpya hutengenezwa bila mahitaji ya mwili. Seli hizi za ziada huendelea kujigawa na kujenga uvimbe (tumors). Saratani za aina nyingi hujenga uvimbe isipokuwa saratani za damu, kama leukemia, ambapo ugonjwa huu huzuia ufanyakazi kazi wa kawaida wa damu kwa kusababisha kugawanyika kwa seli za damu kusiko kwa kawaida.

Uvimbe unaotokana na saratani ni hatari kwa maisha, huweza kuenea kwenye maeneo ya karibu ya mwili na kadiri unavyokua baadhi ya seli huweza kujitoa kutoka eneo moja zikasafiri kupitia mfumo wa damu hadi eneo jingine la mwili na kuanza kujenga uvimbe mpya kwenye eneo hilo jipya mbali kabisa na eneo la awali. Uvimbe wa saratani unaweza kukua na kuvuruga utendaji kazi wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, ubongo na mfumo wa damu. Uvimbe unaotokana na saratani ukiondolewa, huweza kurudia kujijenga upya kabisa.

CHANZO CHAKE

Ni ugonjwa unaotokea katika viini vya mwili vinavyohusika na kurithisha tabia kutoka kizazi kimoja hadi kingine (genes) unaotokana na kubadilika kwa genes zinazohusika na ufanyaji kazi wa seli za mwili, na hasa zile zinazohusika na namna seli zinavyokua na kujigawa.

Mabadiliko katika genes yanaweza kuwa ya kurithi kutoka kwa wazazi au kutokea katika kipindi cha maisha ya mtu kutokana na hitilafu zilizotokea wakati wa kugawanyika kwa seli au kutokana na uharibifu wa DNA uliotokana na vitu vilivyopo kwenye mazingira viitwavyo carcinogens. Vitu vya kwenye mazingira vinavyosaidia kuharibu DNA na kukua kwa kansa (carcinogens) ni kama kemikali zilizopo ndani ya moshi wa tumbaku, asbestos, arsenic, mionzi ya gamma, X-rays, moshi wa magari na mionzi ya jua (UV rays).

Umri wa mtu unapoongezeka, uwezekano wa kutokea dosari katika mabadiliko ya DNA yanayosababisha saratani huongezeka na kufanya umri kuwa ni sababu moja ya kuweza kupata ugonjwa huo kirahisi.

Kuna virusi wanaohusishwa ambao ni human papillomavirus (wanaosababisha saratani ya shingo ya kizazi cervics), hepatitis
B na C (wanaosababisha saratani ya ini), Epstein-Barr virus (anayesababisha baadhi ya saratani za utotoni), Human immunodeficiency virus (HIV) na kitu chochote kinachodhoofisha kinga za mwili

mchanganyiko tofauti wa sababu zilizochangia mabadiliko hayo katika genes zake. Saratani inavyozidi kukua ndivyo mabadiliko ya ziada huongezeka. Uvimbe mmoja unaweza kuwa na seli zilizozalishwa kutokana na aina tofauti ya mabadiliko katika genes.

Kansa iliyoenea kutoka sehemu moja ya mwili ilipoanzia hadi sehemu nyingine huitwa metastatic cancer na tendo la saratani kuenea kutoka sehemu moja hadi nyingine ya mwili huitwa metastasis. Kansa iliyoenea kutoka sehemu moja ya mwili hadi nyingine huwa na aina ya seli zilezile za sehemu ambako ilitokea na hupewa jina lile lile la aina ya kansa ya sehemu ya mwanzo ilikotokea.

Kwa mfano, saratani ya ziwa iliyoenea na kwenda kujenga uvimbe katika mapafu haitaitwa ya mapafu bali metastatic cancer ya ziwa na uchunguzi kwa vyombo maalumu wa seli za sehemu hizi mbili utaonyesha kufanana kwa seli za sehemu hizo mbili toauti. Saratani hizi zinazotokea kwa kuenea kutoka sehemu moja ya mwili hadi nyingine (metastatic cancers) huleta madhara makubwa kwa ufanyaji kazi wa mwili na idadi kubwa ya watu wanaofariki kwa saratani, hufariki kwa sababu ya aina hii ya kansa.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanasema mtindo usio bora wa maisha ikiwamo aina ya ulaji na kutokufanya mazoezi imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa aina mbalimbali za saratani.

Mara nyingi wamekuwa wakitoa elimu ya jinsi ya kubadilisha mfumo wa maisha ili kuisadia jamii.

HALI YA SARATANI NCHINI

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la tafiti za Saratani, kila mwaka kati ya watu 100,000 wagonjwa wapya wa saratani ni 76.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, anasema shirika hilo linakadiria kuwa wagonjwa wapya wa saratani kila mwaka ni 42,060 na katika kila wagonjwa wapya vifo ni asilimia 68, hii inamaana kwamba katika kila wagonjwa 100 wagonjwa 68 wanafariki hivyo jumla ya wagonjwa 28,000 hufariki kwa mwaka.

“Takwimu za hospitali zinazohudumia wagonjwa wa saratani zinaonesha kuna jumla ya wagonjwa 13,216 hii inamaana kwamba wagonjwa wengi wa saratani hawafiki katika vituo vya kutolea huduma na badala yake hubaki majumbani au kwenda kwa waganga wa kienyeji.

“Ni asilimia 31 tu ya wagonjwa wanaofika kupata huduma, tunawahimiza watu wanaohisi kuwa na ugonjwa huo kufika vituo vya kutolea huduma za afya.

“Lakini tatizo lingine ni kwamba hata hao wanaofika hospitali wanakuja wakiwa katika hatua ya mwisho,”anaeleza .

Anaongeza: “Takwimu tulizonazo zinaonesha saratani inayoongoza kwa wanaume ni ya tezi dume ikiwa na asilimia 23, koo na chakula asilimia 16; kichwa na shingo asilimia 12; utumbo mkubwa na mdogo asilimia 11.4 na matezi asilimia tisa.”

“Saratani zinazowakumba wanawake ni mlango wa kizazi asilimia 47; matiti asilimia 16; utumbo mkubwa na mdogo asilimia 5.8; koo asilimia 5.3; na saratani ya kichwa na shingo ikiwa ni asilimia 4.2.

“Takwimu za Ocean Road zinaonesha wagonjwa wengi wa saratani chanzo chake ni maambukizi ya virusi. Zaidi ya asilimia 50 ya wanaume wenye umri kuanzia miaka 30 hadi 49 wamekuwa wakikumbwa na ugonwa huo,” anabainisha Waziri Ummy.

MWONGOZO MPYA SARATANI

Februari 4 mwaka 2017, Shirika la Afya Duniani (WHO) ilizindua mwongozo wa kuwezesha uchunguzi wa mapema wa ugonjwa wa saratani unaotajwa kuwa hatari kwa kusababisha vifo vya watu milioni 8.8 kila mwaka duniani, kati ya wagonjwa milioni 14 wanaobainika kuwa na ugonjwa huo.

shi vya saratani navyo vinaongezeka. Shirika hilo linasema saratani haipaswi kusababisha kifo hasa wakati huu ambapo kuna kampeni za kudhibiti visababishi kama vile matumizi ya tumbaku, unywaji wa pombe na mlo usiofaa.

Februari 3, mwaka huu, Serikali ilizindua mwongozo mpya wa saratani, ambapo Waziri Ummy anasema unaendeleza mapambano makali dhidi ya saratani.

Mwongozo huo umelenga mfumo mmoja wenye ubora wa utoaji huduma za matibabu katika hospitali zote zilizopo nchini na kuhakikisha matibabu bora kwa wagonjwa wote.

Ummy anasema utakuwa na dira ya pamoja kuwaunganisha watoa matibabu.

“Ni matumaini yangu kuwa mwongozo huu utarahisisha mawasiliano kati madaktari bingwa na wataalamu wengine wa saratani kwani unaeleza nini kifanyike kwa nchi nzima kulingana kwa ubora wa matibabu ya saratani.

“Mwongozo unasema kabla mgonjwa hajaanza matibabu wataalamu watakaa kumjadili mgonjwa na kuamua ni jinsi gani waweze kumtibu kisha wanaamua watumie matibabu gani, pia utarahisi uandaaji wa maoteo ya ununuzi wa dawa na vitendanishi vinavyotumika katika kutibu ya saratani,” anasema Ummy.

Anasema kuwa mwongozo huo pia utatoa maelekezo kwa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF), ili vipimo na dawa za saratani viwepo katika vifurushi vyao.

“NHIF uhakikishe unatumia mwongozo huu katika kuweka vitita vya huduma za saratani, hili mliangalie kama kwenye vifurushi mnatoa huduma za CT scan halafu hupati matibabu ndio nini? Nimewaelekeza NHIF waongeze hata fedha kwani mtu anaweza hata kupata tatizo la figo, tuhakikishe watu wanapata matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Dk. Grace Maghembe, anasema mwongozo huo utahakikisha matibabu ya saratani yanatumika bila kuleta madhara.

“Huduma za saratani matibabu yake yanatumia dawa, tindikali, mionzi na hata nyuklia hivi vyote vinahitaji uangalifu ili tuweze kuhakikisha matibabu hayo yanatumika bila kuleta madhara. “Mwongozo unasema kila anayetaka kutoa huduma afuate mwongozo huo kwa sababu unaelekeza namna ya utoaji huduma kuanzia ngazi ya msingi hadi taifa kulingana na aina ya huduma.

UBORESHAJI HUDUMA

Uboreshaji wa matibabu ya saratani hasa ununuzi wa dawa na mitambo ya kisasa umekuwa na nafasi kubwa katika kuwahudumia wagonjwa ndani ya nchi.

Waziri Ummy anasema serikali inaendelea kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na kuwekeza zaidi katika kinga ya saratani.

“Tutaendelea kuchukua hatua za kuboresha huduma za matibabu ya saratani tukiwekeza zaidi katika kinga mfano saratani ya mlango wa kizazi inaweza kuzuiwa kwa chanjo. Takwimu ya mwaka 2018 /2019 zinaonesha kuwa wasichana wa umri wa miaka tisa hadi 14 waliopata chanjo dozi ya kwanza ni 81, huku kwa chanjo ya pili ni asilimia 49 hivyo tutaweka nguvu zaidi.

“Sasa tuna vituo 624 vya huduma za afya vinavyotoa uchunguzi na mabadiliko ya saratani ya mlango wa kizazi, kati ya hivyo 212 ni hospitali, 125 ni vituo vya afya na 286 ni zahanati.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage, anaeleza kuwa ufungaji wa mitambo ya kisasa umeokoa maisha ya wagonjwa wengi na kupunguza rufaa za nje ya nchi.

Dk. Mwaiselage anasema kwasasa wamekuwa na huduma bora ikilinganishwa na awali huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka, hii inachagiwa na wananchi wengi kupata elimu hasa ya kwenda hospitali kupima na kupata matibabu. “Tumepata mashine mbili za mionzi za kutibu saratani, toka mashine hizi zimefungwa Septemba, mwaka jana, tumeweza kuhudumia wagonjwa 1,141.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles