23.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Ukatili, kunyooshewa kidole kunavyorudisha nyuma mapambano ya UKIMWI nchini

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

UKATILI wa Kijinsia na Unyanyapaa wa kunyooshewa kidole umetajwa kama moja ya sababu inayochochea maambukizi ya VVU na Ukimwi nchini ambapo takwimu zinaonyesha kuwa maeneo yalioyo na kiwango kikubwa cha VVU yanasababishwa na matokeo ya kuwepo kwa vitendo hivyo.

Dk. Katanta Simwanza kutoka Shirika la Engender Health Tanzania , akizungumza kwenye warsha hiyo.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni mjini Bagamoyo na Dk. Katanta Simwanza kutoka Shirika la Engender Health Tanzania, kwenye warsha ya kuwajengea uwezo Maofisa Habari na Waratibu wa Ukimwi kutokia Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara iliyoandaliwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanwake(UN-WOMEN).

Kwa mujibu wa Dk. Simwanza matendo hayo ya ukatili wa kijinsia yana uhusiano mkubwa na afya ya jamii na kwamba pamoja na jamii kuhitaji elimu ya VVU pia ya ukatili ni muhimu ili kusaidia kupunguza maambukizi.

“Katika jamii tunayoishi kuna changamoto kubwa sana ya matendo ya ukatili wa kijinsia, tunaona kwamba matendo haya yana mahusiono makubwa sana na matokeo mengine ya afya ya jamii kama maambukizi ya VVU.

“Ukiangalia takwimu zinaonyesha kwamba maeneo ambayo yana kiwango kikubwa cha virusi vya Ukimwi pia yana sababishwa na matokeo ya kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijisnsia kwa kiwango kikubwa sana, ndio maana pamoja na kutoa elimu ya VVU pia tunatoa elimu ya ukatili wa kijinsia.

“Hivyo pamoja na kutoa huduma ya njia za afya ya uzazi pia tunatoa nafasi ya kutoa elimu kwa Wanawake juu ya ukatili wa kijinsia, maambukizi ya VVU na saratani ya shingo ya kizazi,” amesema Dk. Semwanza.

VVU, Unyanyapaa na Ubaguzi

Akizungumzia VVU, unyanyapaa na Ubaguzi, Dk. Semwanza amesema kuwa changamoto ya VVU imezidi kuendelea siku zote sababu ya uwepo wa masuala ya unyanyapaa.

Amesema masuala ya unyanyapaa na ubaguzi yamesababisha watu kukosa fursa ya kupata huduma kwa kuogopa kunyooshewa mikono.

“Pia jamii ikiwamo watoa huduma kwa namna moja ama nyingine kwa kufahamu hali za watu wakati mwingine wahusika wamekuwa wakikosa kupata huduma ndio maana tunasema kuwa ni vizuri kuja na hafua zitakazoanza kuongelea madhara ya unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU.

“Kwa kufanya hivyo itatoa fursa kwa watu wanaoishi na VVU kuweza kujitokeza kwa uwazi zaidi na kupatiwa huduma, kwani tafiti zinaonyesha kuwa vijana wa kike wenye miaka 15 hadi 25 wana kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU.

“Pia tafiti zinaonyesha kwamba kundi hilo hawataki kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya unyanyapaa, kwani wanapoenda kwenye vituo hivyo jamii inaanza kuwanyooshea vidole na kuwauliza ‘wewe bado ni mtoto mdogo umekuja kufanya nini hapa, umekujaje kwenye kliniki ya watu wanaoshi na VVU au ya uzazi wa mpango’wengine wanafikia hatua ya kuambiwa kuwa ‘Tutaenda kuwaambia wazazi au walimu wako kuhusu mambo unayoyafanya hapa, wengine wanambiwa kuwa ‘Unamkosea Mungu kw akufanya haya mamo unayokuja kuyafanya hapa’ hivyon vitu kama hivyo vimekuwa vikileta changamoto na kufanya watu kushindwa kupata huduma za msingi ambazo wanapaswa kupewa,” amesema Dk. Simwanza.

Dk. Simwanza amesema jambo la msingi linalotakiwa kufanyika ni kuvunja UKIMYA na kuelezea madhara ya unyanyapaa na kunyooshea watu mikono ambao wanatumia dawa za VVU au njia za afya ya uzazi.

“Hivyo, tunatakiwa kutoa elimu kwa jamii kwa kutumia watu ambao wanaushawishi mkubwa katika jamii zetu wakiwamo washehereshaji, viongozi wa dini na jamii ambao iwapo wakisimama vizuri na kuzungumzia changamoto hizi basi itasaidia kubadilisha jamii yetu,” amesema Dk.Simwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,248FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles