26.7 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Ujenzi wa kituo mahiri cha zao la ndizi kukamilika

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Taasisi ya Afrika ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imebainisha kuwa ipo katika hatua ya ujenzi wa kituo mahiri cha zao la ndizi.

Kituo hicho kinatajwa kuliongezea thamani na ithibati katika mnyororo wa thamani zao hilo kuanzia kwenye mbegu na uvunaji ili liuzwe kimataifa.

Hayo yameelezwa Oktoba 20,2022 na Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Emmanuel Luoga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji na mwelekeo wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Amesema kituo hicho cha umahiri kitahusisha kitengo cha maabara kitakachosaidia kufanya tafiti za viuatilifu asilia kwenye mazao nchini.

Amesema zao hilo litakisaidia Kiwanda cha kutengeneza mvinyo (Banana wine) kinachotumia ndizi ambacho anadai kina umaarufu mkubwa lakini kina changamoto ya uzalishaji na usambazaji mdogo wa bidhaa hiyo.

“Harakati hizi tunashirikiana na TARI kufanya utafiti wa kupata mbegu bora ya zao la ndizi, na sehemu nyingi zao hili linashambuliwa na magonjwa hususan ya mnyauko kwahiyo tunaendelea kufanya tafiti za mbegu ambazo hazishambuliwi na magonjwa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,694FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles