28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Ujenzi wa daraja Katoro-Kyamlaile wafikia asilimia 95

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Ujenzi wa Daraja linalo unganisha Mawasiliano ya kata ya Katoro,Kashaba,na Kyamlaile wilayani Bukoba mkoani Kagera limefikia asilimia 95 kukamilika.

Daraja hilo lilikuwa limejaa maji kwa kipindi cha miaka mitatu na kusababisha Wananchi wa kata hizo kutumia mitumbwi kuvuka eneo la lenye urefu wa kilometa 1

Akizungumzia ujenzi huo leo Jumatatu Oktoba 25, 2021 Mratibu wa Wakala wa Barabara mjini na Vijiji (TARURA) Mkoa wa Kagera, Avit Theodory amesema mwaka 2018 hadi 2019 eneo hilo lilitengewa bajeti ya Sh milioni 519 kwa ajili ya ujenzi kulingana na eneo hilo kuwa korofi.

Aidha, amesema katika kufanikisha kuzuia maji yaliyokuwa yamejaa kwenye barababara na kutengeza mto ililazimika kujenga tuta lenye umbali wa km 1 pamoja na ukuta kwenye eneo la km 300,ujenzi wa karavati 12 tofauti, kujaza mawe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles