28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Manispaa ya Bukoba yahitaji madarasa 30

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera inaupungufu wa vyumba vya madarasa 30 kwa shule za Sekondari 11 za Kata.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Hamid Njovu wakati akizungumza na Mtanzania Digital ofisini kwake mjini hapo.

Hata hivyo Njovu amesema uhitaji huo unatokana na matarajio ya ufaulu wa wawanafunzi waliosajiliwa na kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu.

Amesema wanafunzi waliosajiliwa ni 3,266 ambapo matarajio ya ufaulu ni 2,939 sawa na wasitani wa asilimia 90.

Kwa sasa vyumba vilivyopo ni 43 vinavyotumika ambapo idadi inayo takiwa Manispaa ni vyumba vya madarasa 73 itakayofanya kila darasa moja kuwa na wanafunzi 40 tu kulingana na sera.

“Niseme tu vyumba hivyo vitajengwa kwenye shule zenye uhitaji mkubwa ili kusawaidia watoto kusoma kwa raha pasipo na msongamano,” amesema Njovu.

Ameongeza kuwa kuna shule zingine hazina maeneo ya kujenga vyumba vya madarasa mfano shule ya Sekondari Bilele inauhitaji wa vyumba vinne lakini imepewa vyumba vitatu.

Kati ya kata hizo 11 kuna shule hazitapata kabisa ambazo ni Bukoba Sekondari, Rumuri, Mgeza, Rutunga, Kagemu pamoja na shule za Kitaifa hazimo katika Mgao.

Kwa upande wake mwalimu Msaatafu Vedasto Cyprian amesema darasa likiwa na wanafunzi wengi mwanafunzi hapati haki ya mwalimu kumkagua mwanafunzi mmoja mmoja ili kutambua uelewa wake.

Mwalimu huyo mstaafu alisema hawezi kutoa zoezi darasani na kusahishia humo maana yake mwalimu atatoa zoezi nakuondoka hivyo si wanafunzi wote watamfanya kazi kwa akili zao wengine wataangalizia kwa wenzao na kufanya mwalimu kuwa kupata picha ambayo sio ya kweli.

Kuna baadhi ya njia za ufundishaji mwalimu hawezi kuzitumia kulingana na wingi wao, mfano kufundisha kwa makundi darasa lilojaa ni ngumu.

“Nitumie tu nafasi hii kuishukuru Serikari kwa kuendelea kutoa pesa kujenga madarasa ili kuwafanya watoto kupata haki yao ya kufundishwa kwa uhuru,” amesema Cyprian.

Naye Diawani wa Kata kashai Ramadhani Kambuga anasema kuwa kulingana na wingi wawakazi wa Kata hiyo wazazi na walezi tushirikiane ili kuwalea watoto kwa maadili iwasaidie kutimiza ndoto zao.

Sasa serikali inatujengea miundombinu ya elimu tushiliki kuwa lea vizuri ili watakapo yatumia madarasa hayo nakuyatunza iwe faida kwa Kizazi hiki na kijacho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles