27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

LATRA Kilimanjaro yakamata magari 212 kwa kukiuka sheria

Safina Sarwatt, Kilimanjararo

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) Mkoa wa Kilimanjaro imekamata magari 212 katika kipindi cha miezi mitatu Julai hadi septemba 2021 kutokana na makosa mbalimbali ya ukikwaji sheria na kanuni za leseni za usafirishaji.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake mjini Moshi, Ofisa Mfawidhi wa LATRA mkoa wa Kilimanjaro, Paul Nyello amesema mamlaka hiyo katika ukaguzi wa magari unaondelea umefanikiwa kukamata magari 212 kwa makosa mbalimbali ya ukikwaji wa leseni za biashara.

Amesema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikiopokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi kuwepo tatizo la ukukwaji wa sheria na kanuni.

Amesema magari hayo yamekamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukatisha ruti bila kufuata sheria,kuingia njia ambayo haziwahusu kutoza nauli ambayo siyo halali tofauti na nauli elekezi mapoja lugha chafu kwa abiria.

Amesema magari hayo yalikamatwa na kupigwa faini kwa mujibu wa sheria za LATRA.

Mbali na hayo mamlaka hiyo pia imewaonya baadhi madereva wanaozidisha abaria, wanatumia lugha chafu kwa abiria na kwamba watachukuliwa hatua za kisheria kwani ni kinyume cha sheria na kutoa wito kwa abiria kutoa taarifa.

Naomba baadhi ya wananchi, Leah Laizer amesema kuwa madereva katika njia za kibosho wamekuwa changamoto kutokana na kutoza nauli kinyume na nauli elekezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles