‘Uhakiki TIN zimebaki siku tisa’

0
651
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo.

NA KOKU DAVID-DAR ES SALAAM

WAKATI zimebaki siku tisa kumalizika  uhakiki na uboreshaji wa namba za Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) kwa mikoa ya kodi ya Dar es Salaam na Zanzibar, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haitaongeza muda tena.

Mamlaka hiyo imesema  badala yake TIN za zamani hazitafanya kazi baada ya muda huo.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema hadi sasa TIN zilizohakikiwa ni 15,467.

Alisema kila mtu mwenye TIN anatakiwa kufika ofisi za TRA kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki  kuepuka kuondolewa katika mfumo wa mamlaka hiyo.

Katika hatua nyingine, TRA imekusanya Sh trilioni 1.37 Septemba mwaka huu, huku lengo lililokusudiwa likiwa ni Sh trilioni 1.4.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here