24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Uganda yazingatia kuwafunga jela wale wanaokataa chanjo ya COVID-19

Kampala,Uganda

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda yanakosoa sheria inayopendekezwa ambayo itawaadhibu watu wanaokataa chanjo wakati wa mlipuko wa maradhi wa hadi miezi sita jela.

Wiki iliyopita, waziri wa serikali wa Uganda anayehusika na biashara alipendekeza marekebisho ya Sheria ya Afya ya Umma ambayo itafini a faini na vifungo vya jela kwa wale wanaokwepa hatua zilizokusudiwa kupunguza kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.

Muswada huo hautaji COVID-19 haswa, lakini bila shaka, COVID-19 ndio ugonjwa ambao nchi na ulimwengu unashughulika nao hivi sasa. Mswada huo unasema kwamba yeyote anayeficha ugonjwa wa kuambukiza anaweza kukabiliwa na faini ya $850 au kifungo cha hadi mwaka mmoja jela.

Wasimamizi wa shule wanaopokea wanafunzi bila ushahidi wa chanjo, au mzazi ambaye atashindwa kuwasilisha mtoto wake kwa ajili ya chanjo, anaweza kufungwa jela hadi miezi sita, faini ya takriban dola 1,100 au zote mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles