23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kiongozi wa mapinduzi ya Mali ajitangaza rais

Bamako, Mali

Kiongozi wa zamani wa Baraza la jeshi nchini Mali, Kanali Assimi Goïta, amejitangaza kuwa rais wa mpito wa baada ya kuwavua madaraka rais wa mpiti na waziri mkuu wa zamani.

Rais Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane sasa wameachiwa huru kutoka kizuizi cha kijeshi.

Wawili hao walipelekwa katika kambi ya kijeshi usiku wa Jumatatu katika hatua ambaye iliifanya Mali kukabiliwa na mapinduzi ya pili ya kijeshi ndani ya miezi tisa.

Hatua hiyo ilichochewa na mageuzi katika baraza la mawaziri ambapo maafisa wawili wa jeshi waliohusika na mapinduzi ya awali walipoteza kazi zao.

Kanali Goïta alilalamika kwamba rais aliyeondolewa madarakani hakushauriana naye kuhusu baraza jipya la mawaziri. Hali ya taharuki imetanda nchi Mali hivi leao lakini kuna utulivu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles