29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Ufaransa yawajibikia mauaji ya kimbari ya Rwanda

Kigali, Rwanda

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema nchi yake ilikuwa na jukumu la kisiasa katika mauaji ya kimbari ya Rwanda na kuwaomba manusura “kuwasamehe” wakati wa ziara yake mjini Kigali leo.

Katua hiyo ilitarajiwa katika hotuba yake katika ukumbi wa makumbusho ya mauaji ya kimbari mjini Kigali, jambo ambalo halikufanywa na watangulizi wake katika kipindi cha miaka 27.

Macron amekiri jukumu la Ufaransa ni “deni kwa wahasiriwa baada ya kimya cha muda mrefu”.

“Kwa kufanya hivyo, wale walionusurika usiku huo, huenda pengine wakatusamehe, (na) kutupatia zawadi ya msamaha,” amesema Macron.

Rais wa Ufaransa ameahidi enzi mpya na kumalizika kwa ‘miaka 27 ya utengano, kutokuelewana na mateso’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles