25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 23, 2021

UCRT yatoa msaada wa vifaa hospitali ya Kiteto

Mohamed Hamad, Kiteto

Shirika la Ujamaa Community Resouce Team (UCRT), lenye makao yake makuu mkoani Arusha, limeikabidhi hospitali ya Wilaya ya Kiteto vifaa vya kujinginga na maambukizi ya ya virusi vya corona kama njia ya kuisaidia serikali kuhudumia jamii

Vifaa hivyo vimetajwa kuwa na thamani ya Sh milioni nne moja ambavyo vitatumika katika mapambano dhidi ya virusi vya corona ambapo imeelezwa kuwa serikali na wadau wameamua kuungana katika vita hivyo ili kunusuru wananchi wake.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Pascal Mbota akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa hivyo amesema msaada huo umefika wakati muafaka ambao hospitali ina uhaba mkubwa wa vifaa hivyo.

“Kila siku natumia laki mbili kwa ajili ya kununua Baracoa, hakuna mtumishi anayekubali kutibu mgonjwa bila kuchukua tahadhari, kwahiyo tuna uhitaji mkubwa sana wa vifaa hivi hasa katika wakati huu,”alisema Mbota.

Akikabidhi vifaa kwa niaba ya shirika hilo, Mwanasheria wa shirika la Ujamaa Community Resource Team, Edward Ole Kaita alivitaja kuwa ni baracoa, madumu ya kunawia mikono, sabuni na vitakasa mikono.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona katika makabidhiano hayo naye alisema kutokana na uhaba wa vifaa katika hospitali hiyo waliomba wadau mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa hatari wa Corona.

“Tunaomba mashirika mengine zaidi yajitokeze kutusaidia hasa katika kipindi hiki..hawamsaidii mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi bali watakuwa wameisaidia jamii ya Kiteto bado tuna changamoto kubwa,”alisema Kambona.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,796FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles