24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Uchumi wa Tanzania wapaa miaka miwili ya Rais Samia – IMF

*Pato la Taifa lafikia Sh trilioni 200 kwa mwaka 2023 kutoka Sh trilioni 163 ya mwaka 2021

*Uchumi wa Tanzania sasa ni mkubwa kuliko baadhi ya nchi za Ulaya na ni wa 6 kwa ukubwa kwa nchi zote za Kusini mwa Jangwa la Sahara

*IMF yabashiri Pato la Taifa la Tanzania kufikia karibu Sh. trilioni 300 ndani ya miaka mitano ijayo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

TAKWIMU mpya za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zinaonesha kuwa Pato la Taifa la Tanzania kwa bei ya sasa limeongezeka hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 85.42 (Sh trilioni 200) kwa mwaka huu wa 2023, ikiwa ni ishara kuwa sera za uchumi za Rais Samia Suluhu Hassan zinaleta mageuzi makubwa nchini.

Ongezeko hilo la Pato la Taifa ni kutoka Dola za Marekani Bilioni 69.9 (Sh trilioni 163.5) kwa mwaka 2021, wakati ambapo Rais Samia alipoingia madarakani.

Rais Samia Suluhu Hassan.

Takwimu hizo za IMF zinaonesha kuwa Pato la Taifa la Tanzania huenda likaongezeka zaidi hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 136.09 (Sh trilioni 276) ifikapo mwaka 2028.

Tangu alipoingia madarakani Machi 2021, Rais Samia ametekeleza sera rafiki kwa sekta binafsi, ambayo imeongeza kasi ya uwekezaji, biashara na ukuaji wa uchumi nchini.

Kwa mujibu wa takwimu hizo mpya za IMF, Pato la Taifa la Tanzania kwa mwaka 2023 ni kubwa kuliko nchi kadhaa ndogo za Ulaya, ikiwemo Croatia ($78.8 billion), Lithuania ($78.3 billion), Serbia ($73.9 billion) and Slovenia ($ 68.1 billion).

Kwa upande wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ni nchi ya 6 kwa ukubwa wa Pato la Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles