31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yadhamiria kuendelea kuzingatia Masuala ya Utawala Bora

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania DSigital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema serikali imeridhia kuwa kifungu maalumu cha bajeti kwa ajili ya kuendesha baraza la Vyama Vya Siasa ili kuweza kufanya shughuli zake kwa ufanisi.

Kauli hiyo imetoloewa wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Vyama Vya Siasa kilichofanyika Mjini Dar es Salaam Aprili 16, 2023. Amesema Serikali imepitisha Bajeti ya Sh 1,586,662,000.00 kwa ajili ya kuendesha Baraza la Vyama vya Siasa kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Pro. Ibrahim Lipumba mara baada ya Ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Vyama Vya Siasa kilichofanyika Mjini Dar es Salaam.

“Kwa kuwa sasa Mhe. Rais Dk. Samia Sulluhu Hassan ameamua kutenga fedha ya kuendesha baraza, naomba vikao vyote vya kikatiba vya baraza la vyama vya siasa vikae kwa kwa mujibu wa ratiba ikiwa ni pamoja na vikao vya kamati kwa kufuata kanuni na sheria,” amesema Mhagama.

Ameongeza kuwa Baraza la Vyama vya siasa lipewe nafasi ya kukutana serikali ili kujadiliana kuhusu mambo mabalimbali yanayohusu ustawi wa Demokrasia nchini.

Iko miradi ya kimkakati hapa nchini, kuna kila sababu viongozi wa vyama vya siasa na baraza la vyama vya siasa wapate nafasi ya kuangalia miradi hiyo kwa sababu tunapofika kwenye masuala ya maendeleo ya nchi na ustawi nchi hakuna chama.

“Kuna nafasi ya viongozi wa vyama vya siasa kutushauri vizuri zaidi kwa ustawi wa wananchi,“ alisema Waziri Mhagama.

Aidha, tunahitaji kutengeneza programu maalumu ya mafunzo kwa ajili ya viongozi wetu wa vyama vya siasa, ili tuendele kuimarisha  Demokrasia ya vyama vingi chini, hatuwezi kufanikiwa kama viongozi wetu hawataendana na mabadiliko yanayoyendelea kwenye ulimwengu wa sasa.

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama ameomba migogoro ya vyama imalizwe ndani ya vyama: “Tunauwezo wa kuimaliza sisi wenyewe, tujenge uwezo wa kutizama matatizo yetu ndani ya chama na kuyamaliza ndani ya vyama vyetu,” amesema.

Waziri amehimiza viongozi wa vyama vya siasa, kuzingatia sheria za matumizi na mapato ya fedha.

Waziri Mhagama ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania.

“Mhe. Rais alipoingia madarakani aliasisi ” 4r” ambazo ni (reconcilian, resiliance, reform and rebuilding) kwa kiswahili ni maridhiano, ustamilivu, mageuzi na mabadiliko hii ikiwa ni kwa lengo la kutoa mwongozo wa jinsi ambavyo siasa za nchi yetu zinapaswa kuwa,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Siasa, Juma Ally Khatibu,  ameomba mfaunzo ya siku  tatu mara tu baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuwa na uelewa mkubwa kuhusu ” 4r”.

Mafanikio ya kikosi kazi katika Mkutano ule uliofunguliwa na Dk. Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma ambao ni zao la Baraza la Vyama Vya Siasa, ni pamoja na kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa,  mafanikio mengine ni kuundwa kwa Tume ya  Rais ya  kuangalia namna ya  kuboresha Taasisi za Haki jinai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles