UCHAGUZI KENYA 2017: MIKE SONKO ATAKA NASA WAPIGWE MAWE

0
522

NA RENATHA KIPAKA,

Mike Sonko amezua mjadala mkali baada ya kuwahimiza wafuasi wake hadharani kuwapiga mawe viongozi wa NASA – Sonko aliwakumbusha wafuasi wake kuhusu kisa cha hivi karibuni mjini Kisumu ambapo Rais Uhuru na Naibu wake William Ruto walihangaishwa na wafuasi wa NASA Seneta maarufu wa Nairobi Mike Sonko, amerejea njia zake za zamani.

Sonko anayetaka kuwa gavana mpya wa Nairobi kwa tiketi ya Jubilee, Julai 14, mwaka huu alitoa matamshi ya uchochezi alipokuwa akihutubia umati katika eneo la Zimmerman, Nairobi.

Mike Sonko aliyekuwa eneo hilo kupigia debe Jubilee alionaswa kwa video akihimiza kundi la vijana waliochangamka kuwapiga mawe viongozi wa National Super Alliance (NASA). Sonko vilevile alirejea kisa cha Kisumu ambapo vijana wahuni walipotishia kumpiga mawe Rais Uhuru Kenyatta.

”Mimi ningependa kuwaambia wajipange. Tuko na polisi, tuko na wanajeshi…Tukiwa hapa kwetu tuwapige mawe…mliona wale walitupia Rais mawe kule Kisumu?” Mike Sonko alihoji. Matamshi ya Sonko yamejiri siku chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kuhangaishwa na wafuasi wahuni wa NASA walipokuwa wakiidhinisha kiwanda cha kupakia cha EABL Kisumu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here