UCHAGUZI KENYA 2017: WANANCHI WAFAHAMISHWA ATAKAYEENDESHA MMDAHALO WA URAIS

0
477

NAIROBI, KENYA

WANAHABARI watakaoendesha mdahalo wa urais utakaofanyika katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki (CUEA), Julai 24, wametangazwa rasmi.

Yvonne Okwara na Joe Ageyo, wote kutoka kituo cha runinga cha KTN na Linus Kaikai wa NTV wametangazwa kuwa wataendesha mdahalo huo unaosubiriwa kwa hamu na wapigakura.

Kaikai ndiye msimamizi wa kituo cha NTV na ana kipindi cha kujadili masuala ya uongozi nchini Kenya.

Naye Joe Ageyo tayari amesimamia midahalo miwili ya ngazi ya ugavana akiwa KTN. Yvone ni mtangazaji wa KTN pia.

Mdahalo wa urais utakuwa Julai 24 baada ya kuahirishwa kutoka Julai 10. Mdahalo wa wagombea wenza unatarajiwa kufanyika Julai 17, ambapo yote itarushwa moja kwa moja katika runinga za Kenya na kuwashirikisha wagombea nane.

Haikubainika sababu ya Hussein Mohammed wa Citizen TV kuachwa nyuma licha ya kuwa maarufu katika mahojiano ya hadhi ya juu.

Wengine waliotarajiwa ni Larry Madowo, Jeff Koinange na Mark Masai. Habari zinasema kuwa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga hawatahudhuria mdahalo huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here