DK. ABBAS KUONGOZA KAMATI YA UCHUNGUZI MKATABA STAR TIMES

0
644
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas

Na Grace Shitundu – Dar es Salaam

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amemteua Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas, kuongoza kamati ya kuchunguza mkataba kati ya Star Times na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), kutokana na utata uliopo.

Kamati hiyo imetangazwa siku moja baada ya Waziri Mwakyembe kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Star Times Group, Xinxing Pang kwa sasa nne na kukubaliana kuunda kamati hiyo itakayopitia mkataba huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasialino Serikalini, Zawadi Msalla, kamati hiyo itakuwa na wajumbe 10, watano kutoka Star Media China na watano kutoka Tanzania.

“Kamati hiyo imepewa hadidu rejea takribani nane na inatakiwa kufanya kazi kwa muda wa siku saba ili kukamilisha kazi hiyo,” ilisema taarifa hiyo.

Katika taarifa hiyo, Msalla amewataja wajumbe wengine kutoka nchini kuwa ni Kyando Evod kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Frederick Ntobi na Mhandisi James Kisaka wote kutoka Mamlaka ya Mawasilano Tanzania (TCRA) na Mbwilo Kitujime wa TBC.

Taarifa hiyo ilisema majina ya wajumbe watano walioteuliwa kutoka Star Media China yatawasilishwa ili kukamilisha idadi ya wajumbe kumi.

Hatua ya kuunda kamati hiyo imekuja baada ya Rais Dk. John Magufuli kumtaka Dk. Mwakyembe kuangalia upya mkataba huo na endapo hauna manufaa afanye uamuzi kwa kuwa kila wakati Star Times inadai kupata hasara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here