22.4 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

UBELGIJI, ENGLAND WATENGENEZA HISTORIA MPYA KOMBE LA DUNIA

SAINT PETERSBURG, URUSI


LEO kwenye Uwanja wa Saint Petersburg, timu ya taifa ya England itashuka dimbani kupambana na Ubelgiji kuwania mshindi wa tatu kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Wawili hao wanakutana baada ya kushindwa kufuzu hatua ya fainali kwenye michezo yao ya nusu fainali ambapo Ubelgiji ilikubali kichapo kutoka kwa Ufaransa, huku England wakifungwa na Croatia.

Hii ni historia mpya kwenye Kombe la Dunia kwa timu mbili za kundi moja kukutana mara mbili kwenye michuano hiyo.

Katika hatua ya makundi timu hizo zilikuwa pamoja kundi G, hivyo zilikutana katika mchezo wa mwisho huku tayari zote zikiwa zimefuzu kuingia hatua ya 16 bora, katika mchezo huo Ubelgiji iliweza kushinda bao 1-0.

Mchezo huo haukuwa na ushindani sana kwa kuwa kila timu ilikuwa imefuzu hatua inayofuata, hivyo makocha walitumia nafasi hiyo kuwachezesha wachezaji ambao hawakupata nafasi kwenye michezo ya awali.

Sasa wanakutana tena leo katika kuwania mshindi wa tatu, huku kesho ikipigwa fainali kati ya Croatia dhidi ya Ufaransa.

Bado England katika historia wanaonekana kuwa wababe kwa Ubelgiji kutokana na jumla ya michezo waliyokutana. Wamekutana mara saba kabla ya mchezo wa leo huku Ubelgiji ikishinda mara moja, England wakishinda mara mbili na kutoka sare nne tangu mwaka 1954.

England leo wanaingia huku wakiwa na mawazo mengi baada ya kushindwa kuingia fainali, walikuwa na matumaini makubwa sana ya kufanya vizuri kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1966 walipotwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Kila mchezaji wa England ameonekana kuwa na kipindi kigumu kutokana na matokea waliyoyapata, baadhi ya wachezaji wamedai hali hiyo inawasumbua kwenye vichwa vyao na itachukua muda kuweza kusahau.

Hali hiyo inaweza kuwafanya wakashindwa kufanya vizuri katika mchezo wao huo wa leo dhidi ya Ubelgiji ambao bado wanaonekana kuwa kwenye hari japokuwa wameshindwa kuingia hatua hiyo ya fainali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,208FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles