23.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Tyga apata mshtuko wa moyo kufiwa na mlinzi wake

2012 BET Awards - Roaming Inside And BackstageNEW YORK, MAREKANI

RAPA Micheal Stevenson ‘Tyga’, amepatwa na mshtuko wa moyo baada ya kupewa taarifa ya kifo cha askari wake ambaye anajulikana kwa jina la Punch Henderson.

Mlinzi huyo wa Tyga alipoteza maisha juzi baada ya gari lake kugongana uso kwa uso na lori ambalo linadaiwa kuwa lilikuwa kwenye mwendo kasi.

Kupitia akaunti ya Instagram ya msanii huyo amedai ameshtushwa na kifo cha mlinzi wake ambaye alikuwa naye muda mfupi kabla ya kifo chake.

“Ni kweli Punch hayupo tena nami? Inawezekana lakini itachukua muda kuamini, ninaamini atakuwa amepata sehemu nzuri ya kupumzika, pumzika kwa amani Punch,” aliandika Tyga huku akiwa ameiweka picha ya mlinzi huyo kama kumbukumbu ya mara ya mwisho kukutana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles