23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wasanii na matumizi ya afya ya uzazi

DSC_2875NA SHABANI MATUTU

TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya T-Marc Tanzania, imeahidi kutoa ajira kwa wasanii wa fani mbalimbali kwa nia ya kuwaelimisha kujikinga na maambukizi ya Ukimwi na uzazi wa mpango.

Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania, Diana Kisaka, aliyasema hayo juzi kwenye uzinduzi wa jengo jipya na ghala ambapo alisema wamekuwa wakiwatumia wasanii kuhamasisha wananchi matumizi sahihi ya kondomu za kike na za kiume.

“Kuanzia mwaka 2004 tulipoanza tumefanikiwa kuajiri watu zaidi ya 600 kwa ajira za kudumu na ajira isiyokuwa rasmi. Kwa mfano leo tumetoa ajira isiyokuwa rasmi kwa kikundi cha ngoma za asili cha ‘Wanne Star’ wanaofanyakazi ya kuburudisha na kutoa elimu ya kutumia kondomu za Dume na Pepeta,” alisema Diana.

Jengo hilo la T-Marc Tanzania lilizinduliwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangallah, aliyekuwa mgeni rasmi akiwakilisha Serikali katika tukio hilo kubwa na la kihistoria.

Awali, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukagua mabanda ya maonyesho ya miradi mbalimbali ya taasisi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles