23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Indonesia yamchunguza Di Caprio

Leonard Di CaprioJAKARTA, INDONESIA

WIZARA ya Uhamiaji nchini Indonesia, imesema inaweza kumfungia msanii wa filamu nchini Marekani, Leonard Di Caprio, kuingia nchini humo kutokana na ujumbe wake wa kuzuia kukata miti ovyo.

Wiki iliyopita msanii huyo alikuwa nchini Indonesia, mara baada ya kurudi nchini Marekani kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii aliandika ujumbe wa kupinga ukataji miti ovyo.

Aliandika kwamba ‘mfumo wa utengenezaji mafuta kupitia ukataji wa michikichi unahatarisha maisha ya wanyama ambao wanaishi porini kutokana na miti hiyo kama vile chui, tembo na vifaru.

Kutokana na kauli hiyo, msemaji wa Waziri wa Uhamiaji amesema iwapo ujumbe huo wa Di Caprio utawekwa kama uchochezi nchini humo basi msanii huyo atazuiwa kuingia tena nchini humo.

Hata hivyo, mshindi huyo wa tuzo za Oscar, amesema hakuwa na maana tofauti kama watu wanavyodhani, ila alikuwa ameyaandika hayo kwa kuwatetea viumbe hai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles