29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Tuzo za Grammy zilivyotikisa

taylor-swiftBADI MCHOMOLO NA MITANDAO

TUZO za Grammy mwaka 2016 kwa awamu ya 58, zilitolewa mwanzoni mwa wiki hii mjini Los Angeles nchini Marekani, huku baadhi ya wasanii wakionekana kung’ara kwa kutwaa tuzo nyingi.

Hata hivyo, mwenzi mmoja kabla ya kufanyika kwa tuzo hizo, kuna baadhi ya wasanii na wadau mbalimbali wa muziki duniani walizikosoa kwa kudai kwamba zina ubaguzi ambapo zinaonesha wazi kwamba wasanii wenye ngozi nyeusi hawakupata nafasi ya kuwania ingawa majina yao yalikuwa kwenye utoaji wa tuzo hizo.

Tuzo hizo zilifanyika Jumatatu wiki hii huku mshereheshaji akiwa mkali wa muziki wa hip hop, Cool J.

Katika tuzo hizo kuna baadhi ya mambo yalijitokeza kama ifuatavyo:-

Selena kumsapoti Beiber

Justin Beiber na Selena Gomez inajulikana kama hawapo pamoja katika uhusiano wa kimapenzi, lakini katika tuzo hizi, Selena aliwashangaza watu baada ya mpenzi wake huyo wa zamani kushinda tuzo ya uchezaji bora kutokana na wimbo wake wa ‘Where are U now’.

Mbali na Selena kuonesha tabasamu aliamua kumpongeza msanii huyo kwa ushindi huo wa mara yake ya kwanza.

Wimbo wa Adele wakwama

Adele ni msanii ambaye ameanza mwaka vizuri kutokana na kutikisa dunia katika tasnia ya muziki na wimbo wake wa ‘Hello’, lakini katika tuzo hizo alipata nafasi ya kufanya shoo na mashabiki walishangaa kuona wimbo wa msanii huyo kukwama kwama na kuwa haueleweki.

Lakini alitumia uzoefu wake na kuimba bila ya biti ambalo lilionekana kuwa tatizo. Hata hivyo, kupitia mtandao wa Instagram, aliwaomba radhi mashabiki wake na kudai kwamba tatizo lilikuwa ni vyombo na sio yeye.

Kendrick, Taylor Swift wafunika tuzo

Mkali wa hip hop, Kendrick Lamar na Taylor Swift, walifanikiwa kufunika katika uchukuaji wa tuzo hizo, ambapo Kendrick akifanikiwa kutwaa tuzo tano ambazo ni albamu bora ya rap, rapa bora, wimbo bora wa rap, wimbo bora wa kushirikisha, mchezaji bora wa rap. Huku Taylor akichukua tuzo tatu, hata hivyo kuna baadhi ya wasanii ambao walifanya vizuri kwa kujichukulia tuzo hizo kama vile Mark Ronson na Bruno Mars kutokana na wimbo wao wa ‘Uptown Funk’ na kufanikiwa kutwaa tuzo tatu.

Lamar amedai kwamba ataendelea kufanya muziki wenye viwango vya hali ya juu ili kuweza kujizolea tuzo mbalimbali duniani.

“Kwenye muziki kuna ushindani wa hali ya juu kikubwa ni kujituma na kufanya kile ambacho mashabiki wanakitaka na ndivyo ninavyofanya na nitaendelea kufanya hivyo,” alisema Lamar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles