23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

‘Tutaendelea kusimamia dira na maelekezo ya Serikali’-Lubuva

Safina Sarwatt, Mwanga

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Zefrin Lubuva amesema halmashauri hiyo itaendelea kusimamia Dira na Maelekezo yaliyotolewa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kuzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za ukusanyaji wa mapato.

Lubuva ametoa kauli hiyo Aprili 24,2021 wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, ambapo amesema kuwa kama halmashauri hiyo wameyachukua maagizo na maelekezo yote ambayo yitolewa na Rais Samia Bungeni Dodoma wakati akilihutubia Taifa kwa mara ya kwanza ateuliwe kuongoza nafasi hiyo, akiwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo ya juu.

Amesema halmashauri ya Mwanga imekuwa ikizingatia ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa kufuata Sheria kanuni na taratibu bila kumuumiza mwananchi jambo ambalo limeweza wananchi kuona umuhimu wa ulipaji kodi kwa hiari na hivyo kupeleka kupata Hati Safi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uliofanika mwaka 2019/2020.

“Hotuba ya Rais Sami, imeeleza mambo mengi hususani kwenye suala la uadilifu na uaminifu katika kusimamia fedha zinazoletwa za miradi ya maendeleo pamoja matumizi sahihi ya fedha za Serikali,”amesema Lubuva.

Aidha Mkurugenzi huyo pia ametoa wito kwa Watendaji kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ili halmashauri hiyo iweze kufanya vizuri zaidi katika kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kuendelea kuilinda Hati hiyo.

“Katika taarifa iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali {CAG} na kutolewa Machi mwaka huu Halmashauri yetu tumepata Hati Safi katika ukaguzi uliofanyika mwaka 2019/2020 hii ni kutokana na uzingatiaji wa Sheria katika ukusanyaji wa mapato na usimamiajia wa mzuri wa miradi ya mbalimbali ya maendeleo,” Mtendaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles