23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tumieni redio kubuni vipindi vinavyoleta tija kwa wananchi

Na Anna Luhasha, Mwanza

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Radio Duniani, Serikali mkoani Mwanza imewakumbusha wasimamizi wa radio kubuni vipindi ambavyo vinaleta manufaa kwa wananchi.

Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel wakati akizungumza na wanahabari katika kuelekea siku ya radio duniani Februari 13.

“Niwaombe wasimamizi na waandaaji wa vipindi vya radio kuagazia mambo ya muhimu yatakayoleta Chachu ya maendeleo kwa wananchi wetu, mfano Serikali inatoa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na walemavu wafikieni hawa wanufaika kujua faida na changamoto zao pindi wanapokopeshwa,” amesema Mhandisi Gabriel.

Nao baadhi ya washiriki katika kongamano hilo akiwemo Jimmy Luende na Dotto Bulendu wamependezwa na namna na mfumo wa Shirika la Internews kuwakutanisha baadhi wasimamizi wa vituo vya radio na waandishi mkoani Mwanza na kuwakumbusha mambo mbali mbali katika tasnia ya habari.

“Tunawashukuru Internews kuona jinsi gani tunapoelekea katika maadhimisho haya kutukutanisha na kuweza kuzungumzia namna ya kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii hasa kwa kufuata misingi ya utangazaji na uhandishi wa habari,” amesema Bulendu.

Mwakilishi kutoka Internews Shabani Maganga amewata waandishi kutumia siku hiyo kuzungumzia siku ya maadhimisho hayo Kama ilivyo kwa maadhimisho mengine ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu ni Radio na uaminifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles