23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tumia SmartPhone kulinda gari lako  

trackr_bravo_with_phone_webNa FARAJA MASINDE

TEKNOLOJIA inazidi kuchukua nafasi kwenye maisha yetu, hii inatokana na kasi kubwa ya uvumbuzi unaoendelea kufanywa na wataalamu kila iitwapo leo.

Je, umeshawahi kwenda mahali ambapo kuna magari mengi tena yanayofanana na lile la kwako kisha ukajikuta hujui ni wapi lilipo gari lako?

Kama hivyo ndivyo basi tambua kuwa kwasasa kuna kifaa maalumu kilichotengenezwa ili kuhakikisha kuwa unalitambua gari lako hata likiwa katikati ya magari 100 yanayofanana.

Kifaa hicho kimetengenezwa na kampuni ya Califonia ya nchini Marekani ambapo kinafanana na ‘alam’ kwa ajili ya kukusaidia kutambua gari lako popote pale unapokuwa.

Kifaa hiki kinajulikana kama, TrackR App, hii ni application ambayo imetengenezwa maalumu kulinda gari lako bila ya kuwa na usumbufu wowote.

Lengo la kifaa hiki ni kukusaidia pindi unapokuwa kwenye mkusanyiko wa watu wengi wenye gari zinazofanana.

Na pia iwapo inatokea uko mahali ambapo unashindwa kujua gari yako ilipo basi kifaa hiki kinaweza kukuonyesha moja kwa moja kupitia ramani iliyoko kwenye app hiyo ambapo utafanya yote hayo kwa kutumia simu yako ya SmartPhone kwa kupakua app hiyo (Dowload).

Mara baada ya kuwa na software ya program hiyo kwenye simu yako kwa maana ya App, unaweza kuambatanisha kifaa hicho kwenye funguo zako za gari au hata kuweka kwenye begi lako, pochi ndogo na sehemu yoyote ambayo unafikiri huwezi kukisahau.

Tofauti na ilivyo kwa huduma ya mfumo uliozoeleka wa kulinda gari wa GPS au tracking, wabunifu hao wanasema kuwa wametambua namna ambavyo huwa inachosha kutumia gharama kubwa kwa ajili ya usalama wa gari lako, kwani kifaa hicho kinakupa taarifa pindi gari lako linapojaribu kuibiwa au mtu kuiba vifaa vilivyoko ndani ya gari yako.

Ili kuunganisha na gari yako unaweza kuhifadhi kifaa hiki sehemu yeyote ambacho kitakuwa kimeunganishwa na simu yako moja kwa moja kupitia program maalumu ambayo ina ramani ndani yake.

Kifaa hiki kiko mbioni kuwasili Afrika ambapo kitapatikana kwa dola 29 tu sawa na Sh 60,000.

Tayari vifaa milioni 1.5 vimenunuliwa duniani kote ambapo kila pakti huambatana na vifaa vinne hivyo, viwili unaweza kuweka popote pale.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles