21.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 5, 2022

Tuendelee na utulivu huu hadi Oktoba 28

Na SALOME BRUNO (TUDARCo)

WATANZANIA wako katika kipindi cha kampeni kuelekeo Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Katika hilo wagombea wa vyama mbalimbali kulingana na nafasi zao wanaendelea kufanya kampeni za kunadi sera ili kuweza kupata ridhaa ya wananchi pindi itakapowadia siku ya kupiga kura.

Ni jambo la kujivunia kuona kwamba kampeni zinaendelea kufanyika kwenye hali ya amani na utulivu.

Kwani hadi sasa hakuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani ambavyo vimeripotiwa, hii ni ishara kwamba jeshi la polisi limeendelea kufanya kazi yake vyema hatuna budi kulipongeza.

Kwani tunashuhudia kuwa katika mikutano ya kampeni jeshi hilo limekuwa mstari wa mbele katika kuahikikisha ulinzi na usalama wa viongozi wa vyama, wagombea pamoja na wananchi wanaofika kusikiliza sera hizo bila kujali chama cha upinzani au chama tawala.

Hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kulipongeza jeshi letu kwa namna ambavyo amani imeendelea kutamalaki tofauti na matarajio ya hapo awali baada ya kushuhudiwa matukio kadha wa kadha ambayo yalikuwa yakihushishwa na siasa.

Matukio hayo yalikuwa ni ya baadhi ya wagombea kudaiwa kupigwa na mambo mengine yenye kufanana na hayo, dalili ambazo ziliacha kuchochea baadhi ya watu kuamini kuwa kusingekuwa na utulivu kipindi hiki cha kampeni.

Hivyo utulivu huu ingekuwa vyema zaidi iwapo ungeendelea mpaka siku za uchaguzi na hata baada ya hapo ili kudumisha amani na usalama wa nchi yetu.

Pia ni jambo la kupongezwa kwa baadhi ya viongozi wa dini hapa nchini ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kuhamasisha amani miongoni mwa watanzania hususani kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu.

Kwani mbali na jeshi la polisi kusimamia ulinzi lakini pia dini nazo zina mchango mkubwa katika kuhamasisha na kuhubiri amani nchini.

Hivyo ni jukumu lao kuhimiza amani na kudumu kwenye upendo siku zote.

Ni matumaini yangu kuwa utulivu huu utaendelea na Tanzania itabaki na amani licha ya uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,680FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles