23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

TRUMP KUZUNGUMZA NA KENYATTA

NAIROBI, KENYA


RAIS wa Marekani, Donald Trump, amepanga kuzungumza kwa simu na Rais Uhuru Kenyatta.

Mazungumzo yao yatakuwa ya kwanza tangu rais huyo wa Marekani apate ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Kenyatta atakuwa rais wa nne wa Afrika kuzungumza na rais huyo kutoka taifa lenye uwezo mkubwa duniani.

Kati ya marais wa Afrika aliozungumza nao kwa njia ya simu ni Rais wa Misri, Abdel Fatah al Sisi, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari.

Awali kitendo cha Trump kuzungumza na marais hao wengine na kuiacha Kenya, kilionekana kuleta hali ya sintofahamu nchini hapa.

Lakini duru za kidiplomasia mjini Washington, zilisema kitendo cha Trump kuikacha Kenya kinatokana na kushindwa kwa diplomasia ya nchi hiyo kwa kutochombeza uwezekano wa kuzungumza naye.

Miongoni mwa masuala ambayo Trump na Kenyatta wanatarajiwa kugusia, ni usalama wa Somalia na ukame unaoendelea kukumba eneo zima la Afrika Mashariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles