24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

HUAWEI YAPEWA TUZO YA UBORA

BARCELONA, HISPANIA


KAMPUNI ya Huawei kupitia kitengo chake cha Active Antenna Unit (AAU), imeshinda tuzo ya simu yenye mfumo bora zaidi katika Mkutano wa Wadau wa Mawasiliano (MWC) 2017.

Tuzo hiyo ilitambua mchango wa Huawei katika ubunifu wa teknolojia na mfumo wake wa mawasiliano na kuimarisha kituo chake kwa vizazi vijavyo.

Katika maonyesho hayo ya siku tano yaliyoanza mwishoni mwa mwezi uliopita na kumalizika juzi, Huawei ilionyesha bidhaa zake mbalimbali za mfumo wa ndani wa mawasiliano.

Kitengo cha AAU, ambacho ni mwendelezo wa uvumbuzi kufikia mahitaji ya watumiaji wa mtandao katika maeneo tofauti, kilianzisha mfumo huo ili kuwezesha upatikanaji wa huduma ya redio kutoka vituo mbalimbali.

Aidha mfumo wa Huawei wa AAU ndio unaoongoza katika mabadiliko ya matumizi ya mtandao.

Na hivyo kuwapo kwa mfumo mpya wa 5G, AAU wa Huawei umerahisisha zaidi na watumiaji hupata video zenye ubora.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Huduma za Mtandao wa Huawei, Zhou Yuefeng, huduma hiyo itaendelea kuboreshwa taratibu kadiri mabadiliko ya kimtandao yanavyoendelea.

“Huduma mpya kama vile VR, HD Video na mtandao wa wirelesss kwa matumizi ya nyumbani, vyote vimesababisha kuwapo na hitaji kubwa la kuimarisha uwezo wa mitandao,” alisema Yuefeng.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles