28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Trump atishia kufunga mpaka Marekani na Mexico

WASHINGTON, Marekani

RAIS  Donald Trump ametishia kufunga mpaka wa  nchi hii  na Mexico ikiwa majirani zake hao  hawatachukua hatua madhubuti kuwazuia wahamiaji kuingia nchini hapa, jambo ambalo linatishia kupoteza biashara yenye thamani ya mabilioni ya dola.

Tishio hilo limetolewa  baada ya kuwapo   wimbi kubwa la wahamiaji wanaoingia nchini humu  wakitokea Mexico kwa nia ya kutafuta hifadhi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Rais Trump alisema   kuna uwezekano mkubwa atafunga mpaka huo wiki hii na kwamba jambo hilo kwake ni sawa tu.

Alisema ni rahisi   kwa Mexico kuzuia watu kuingia Marekani lakini haijaamua kufanya hivyo’.

Rais Trump hivi karibuni aliandika mfululizo ujumbe wa twitter ambao alihitimisha kwa kusema   Marekani inapoteza fedha nyingi kwa ajili ya wahamiaji, hasa unaposhughulikia na suala la uingizaji wa dawa za kulevya   na hivyo kwa  kufunga mpaka litakuwa jambo jema!”

Trump pia alitoa maelekezo kukata misaada kwa El Salvador, Honduras na Guatemala ambako wahamiaji wengi wanatokea.

Hata hivyo Rais L√≥pez Obrador alisema   suala la wahamiaji  si la Mexico.

Alisema tatizo hilo limeota mizizi katika eneo la nchi za Amerika ya kati zaidi kuliko Mexico.

”Raia wa Mexico hawatafuti tena kazi  Marekani. Wengi wa wahamiaji wana asili ya nchi za Amerika ya Kati,” alisema Rais Obrador.

”Ninataka kuweka wazi kuwa hatutagombana na serikali ya Marekani, upendo na amani,”alisema  Rais Lopez katika mkutano wake na waandishi wa habari kufuatia kauli ya Rais Trump.

Alizungumzia kuhusu uhamiaji ni  kuwa ni haki ya mwanadamu na akasema kuwa watu wa Amerika ya Kati hawana namna ya kufanya hivyo wanatafuta namna ya kupata maisha bora.

Waziri wa Mambo ya Nje, wa Mexico, Marcelo Ebrard amesema kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa Mexico ni  jirani mzuri’ kwa Marekani ”lakini haitachukua hatua kutokana na vitisho”

 Vyombo vya usalama vilifanya doria na vimekua vikishuhudia idadi kubwa ya watu wanaotafuta hifadhi wakikimbia machafuko El Salvador, Honduras na Guatemala.

Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani walisema  idadi ya  Machi ilitegemewa kuwa 100,000 ambayo ni kubwa  zaidi katika kipindi cha miaka 10 .

Hata hivyo haijulikani ni kwa namna gani kufunga vituo vya kuingilia kunaweza kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia nchini hapa  ikizingatiwa kuwa wengi hupitia kwenye vituo visivyo rasmi na kuanza kufuata sheria za kuomba hifadhi wakati tayari wakiwa wameingia kwenye ardhi ya Marekani.

Kwa mujibu wa maofisa wa sensa, kufungwa mpaka kunaweza kuathiri uchumi kwenye nyanja za utalii na biashara kati ya Marekani na Mexico, ambayo ilifikia pauni bilioni 469 mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles