31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KUNA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA EBOLA DRC-WHO

Shirika la Afya duniani WHO limetoa ripoti katika tovuti yake ikisema wiki hii kumekuwa na ongezeko la maambukizi ya mlipuko wa Ebola unaoendelea nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika eneo la Kivu Kaskazini na Ituri.

Katika kipindi hiki vikundi vya wataalamu wa kudhibiti Ebola vinakabiliana na changamoto za kila siku katika kuhakikisha utambuzi kwa wakati na ufuatiliaji wa maambukizi yote katikati mwa vurugu za makundi yenye silaha na pia kutoaminiana miongoni mwa jamii zilizoathirika.

Hata hivyo WHO inasema hatua zimepigwa katika maeneo kama Mandima, Masereka na Vuhovi ambako taratibu timu za watalaamu waliko huko zimeweza kwa mara nyingine na kwa kukubalika na jamii kukata mnyororo wa maambukizi.

Taarifa ya WHO inaeleza kuwa katika siku 21 zilizopita yaani kuanzia tarehe 6 hadi 26 ya mwezi Machi, jumla ya visa 125 vya maambukizi mapya vimeripotiwa kutoka katika vituo 51 ndani ya maeneo 12 kati ya 21 yaliyoathirika hadi sasa. 

Asilimia 38 ya maeneo 133 yaliyo chini ya uangalizi imeathirika. Idadi kubwa ya walioathirika wanatoka katika maeneo ya Katwa (36), Butembo (14), Mandima (19), Masereka (18) na Vuhovi (17).

Hadi kufikia Machi 26, jumla ya visa 1029 vilivyothibitika na visivyothibitika, vimeripotiwa ambapo kati ya watu hao, 642 wamepoteza maisha. Kati ya visa 1029 vilivyoripotiwa, asilimia 57 yaani watu 584 walikuwa wanawake na asilimia 30 yaani watu 307 walikuwa watoto chini ya umi wa miaka 18.

Idadi ya wahudumu wa afya walioathirika imepanda hadi kufikia 78 sawa na asilimia 8 ya maambukizi, vikiwemo vifo 27. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles