TRUMP ARUSHA VIDEO ‘AKIIPIGA’ CNN

0
935
RAIS wa Marekani Donald Trump
RAIS wa Marekani Donald Trump

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani Donald Trump amerusha video katika mtandao wa Twitter ikimuonyesha akimpiga mtu mwenye nembo kichwani ya Shirika la Habari la CNN.

Video hiyo iliyofanyiwa ukarabati ni ile inayomuonyesha Trump wakati alihudhuria michezo ya mieleka ya Shirika la Mieleka la WWE mwaka 2007, ambapo ‘alimshambulia’ mmiliki wa michezo hiyo Vince McMahon.

Video hiyo iliwekwa katika mtandao unaomuunga mkono Trump mapema wiki hii.

 

CNN baadaye ilimlaumu Rais kwa kuibua ghasia dhidi ya vyombo vya habari.

Mchambuzi mmoja katika Kituo cha Habari cha ABC Ana Navarro, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Trump, alisema kuwa video hiyo ni uchochezi na huenda ikasababisha waandishi kuuawa.

Lakini mshauri wa masuala ya usalama nchini Marekani Thomas Bosset, ambaye awali alihojiwa na kituo hicho alidai video hiyo haionekani kuwa tishio.

Mara kwa mara Rais Trump amekuwa kwenye mzozo na CNN analoliita ‘taarifa bandia’

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here