QATAR YAONGEZEWA SAA 48 KUTEKELEZA MASHARTI YA NCHI ZA KIARABU

0
442
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani

KUWAIT CITY, KUWAIT

SAUDI Arabia na washirika wake wa Kiarabu zimeongeza muda kwa nchi ya Qatar, kutimiza masharti iliyopewa la sivyo iwekewe vikwazo zaidi baada ya saa 48.

Tarehe ya mwisho ya kuitaka Qatar kukubali masharti 13, ikiwemo ya kukifunga Kituo cha Utangazaji cha Al Jazeera ilimalizika juzi.

Taifa hilo la Ghuba lilisema litajibu kupitia barua ambayo ilitarajiwa kuwasilishwa kwa Kuwait jana.

Qatar inakana madai kutoka kwa majirani zake kuwa inafadhili itikadi kali.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani alielekea Kuwait jana kuwasilisha barua hiyo kutoka kwa Kadhi wa Qatar kwenda kwa Kadhi wa Kuwait ambaye ndiye mpatanishi mkuu wa mzozo huo.

Aidha Jumamosi iliyopita, Al-Thani, alisema kuwa taifa hilo lilikataa masharti hayo lakini liko tayari kwa mazungumzo.

Qatar imekuwa chini na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa wiki kadhaa sasa, kutoka kwa Saudi Arabia, Misri, Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo kufadhili makundi ya kigaidi na kuingilia masuala ya jirani zake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here