24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM YAMVAA SUMAYE

Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye

Na Mwandishi Wetu-Morogoro

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM), umesema Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, hafahamu wala hajui dhana ya demokrasia ya vyama vingi,  jambo linalomfanya kiongozi huyo kila siku kuilaumu Serikali.

Kauli hiyo ya UVCCM, imekuja siku chache baada ya Sumaye kudai kwamba watawala wa Serikali wa sasa wanaiogopa Katiba Mpya na kugeuka kuwaandama wapinzani kwenye mfumo wa vyama vingi.

Hayo yalisemwa jana mjini hapa na Kaimu  Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akizungumza na vijana wa CCM Mvomero wakati akielekea mkoani Dodoma ambapo alisema hatua hiyo ya Sumaye ya kudai kuna mfumo mgumu wa demokrasia haileti mantiki kwa sasa.

Alisema msingi wa kuruhusiwa vyama vingi nchini si kukwamisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii au kuwafanya wananchi kila siku wakusanyike viwanjani kusikiliza mikutano ya hadhara bila kutilia maanani uzalishaji mali viwandani, mashambani na maofisini.

“Vijana wenzangu hata ligi ya soka au mashindano ya kutafuta warembo yana msimu na vipindi vyake, timu haziwezi kushiriki michuamo mwaka mzima bila wachezaji na waamuzi kupumzika, domokrasia ya wapi ambayo haina vipindi vya kampeni.

“…uchaguzi au watu kutakiwa kufanya kazi za maendeleo acheni kusikiliza poroja za wanasiasa waliochoka vijana chapeni kazi sasa ili kujiletea maendeleo endelevu,” alisema Shaka .

Alisema UVCCM imeshangazwa na matamshi ya Sumaye anayedai kuwa serikali ya awamu ya tano inakandamiza  misingi ya demokrasia kwasababu tu imevitaka vyama kuendesha shughuli za kisiasa kwenye mikutano ya ndani ili kuwapa nafasi wananchi kujituma na kuzalisha.

Kaimu huyo Katibu Mkuu alisema hata kanuni na fomula za masomo ya hesabu, kemia na baiolojia hazilingani katika kupata majawabu halisia hivyo akataka ifahamike  demokrasia nayo ina vipindi vya kampeni , mikutano ya hadhara, uandikishaji, upiga kura, kuhesabu na kutangazwa matokeo .

“UVCCM tunamfahamu Sumaye toka akiwa Naibu Waziri wa Kilimo hadi Waziri Mkuu, hana rekodi nzuri ya kiutendaji ilioleta tija, mafanikio au ufanisi katika maeneo  aliyoyaongoza, yaonyesha ni mshabiki wa hadithi kuliko kufanya kazi,” alisema.

Kutokana na hali hiyo alimtaka mwanasiasa huyo kufuta ndoto na fikra siku moja itatokea CCM kudondoka madarakani kisha yeye au mshirika wake Edward Lowassa mmoja kati yao awe urais wa Tanzania.

“Tanzania imechoka kuwa ombaomba wa kila msaada toka kwa wahisani na washirika wa maendeleo, Serikali ya CCM  imezinduma usingizini na kujitambua, haitaruhusu upuuzi usio na manufaa ili ionekane demokrasaa maana yake ni mikutano ya hadhara bila uzalishaji mali,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles