32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Trump akatisha mahojiano kisa msaidizi wake kakohoa

WASHINGTON-MAREAKANI 

MAHOJIANO yaliyofanywa Jumapili kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na kituo cha ABC News yalikatishwa kwa muda, baada ya msaidizi wake kukohoa kwa bahati mbaya jambo ambalo lilimkera rais huyo.

Wakati Rais Trump akizungumzia juu ya taarifa za fedha, Katibu Mkuu wake, Mick Mulvaney, kwa bahati mbaya alikohoa.

Rais Trump alionekana kuchukizwa na kitendo hicho na kusimamisha mahojiano hayo.

Trump  alisema; “Hebu tufanye basi, anakohoa katikati ya taarifa yangu. Sipendi, unajua, sipendi kabisa.”

Tangu alipoanza kampeni mwaka 2016 Trump amejikuta katikati ya moto kwa kutotoa taarifa zake za fedha. 

Wakati akizungumzia juu ya utawala wake hata katika siku za hivi karibuni aligoma kuweka hadharani rekodi zake, akisema; “ kuna muda natumaini wanazipata kwa sababu ni taarifa nzuri mno za fedha.”

Wakati mafundi mitambo wakiweka sawa ili mahojiano hayo yarejee tena, Trump alimuonya Mulvaney akisema; “Kama utakohoa, tafadhali ondoka. Kama huwezi, huwezi kukohoa sawa.”

Trump alilazimika kurudia tena taarifa yake juu ya kutotoa rekodi zake za kodi wakati mahojiano yalipoanza tena.

Kitendo  hicho cha kusimamisha mahojiano kiliibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter.

Brit.@Bretana_ aliandika katika mtandao huo akihoji hivi ni kweli huyu jamaa kakasirika kwa sababu ya mtu fulani kukohoa!?

Jude @truejbru naye aliandika; kila ninapomuona anaongea nakasirika kwa sababu watu kweli walimpigia kura huyu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles