TRUMP AGAWA KIHOLELA NAMBA YAKE YA SIMU

0
819
RAIS wa Marekani, Donald Trump

 

 

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump, anadaiwa kugawa hovyo namba yake ya simu ya mkononi kwa viongozi mbalimbali wa dunia, akiwaambia wanaweza kumpigia moja kwa moja kinyume na itifaki.

Hatua hiyo isiyo ya kawaida si tu inavunja itifaki ya kidiplomasia, bali pia inazusha wasiwasi wa usalama na usiri wa mawasiliano ya Amiri Jeshi Mkuu huyo wa Marekani.

Maofisa wa Marekani wa zamani na wa sasa walio na uelewa na tabia hiyo, wamesema Trump amewataka viongozi wa Canada na Mexico kumpigia simu moja kwa moja kupitia simu yake ya mkononi.

Kwa mujibu wa maofisa, kati ya viongozi hao wawili, ni Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau ambaye ametumia mwanya huo.

Trump pia alibadilishana namba na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron wakati walipozungumza kufuatia ushindi wake mapema mwezi uliopita.

Hayo ni kwa mujibu wa ofisa wa Ufaransa, ambaye hakutaka kueleza ikiwa Macron alikuwa na dhamira ya kuitumia namba hiyo ya simu.

Dhana ya viongozi wa dunia kuwasiliana kupitia simu inaweza kuonekana kama jambo la kawaida katika ulimwengu wa sasa wa simu za mkononi.

Lakini katika uwanja wa kidiplomasia, ambako mawasiliano ya simu kati ya viongozi ni masuala yanayofuata taratibu, huo ni uvunjaji mwingine wa itifaki kwa rais ambaye ameeleza kukosa imani na njia rasmi za mawasiliano.

Utaratibu na nidhamu ya kufuata itifaki za kidiplomasia limekuwa ni jambo gumu kwa Trump, ambaye hata kabla ya kuingia madarakani, alikuwa anapatikana kwa urahisi na kujiona kuwa mtu aliye huru kutofuata taratibu za kawaida na mtu aliye na ujuzi wa kufikia makubaliano ya biashara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here