26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE AHOJI FEDHA UJENZI WA HOSPITALI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo

 

 

Na Ramadhan Hassan,

MBUNGE wa Singida Mjini, Musa Sima (CCM), amehoji Serikali ina makakati gani wa kutoa fedha kujenga Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.

Akiuliza swali la nyongeza jana bungeni, Sima alidai kuwa Serikali iliahidi kutoa Sh bilioni 1.7, lakini hadi sasa imetoa Sh bilioni moja. Je, fedha zilizobaki zitapelekwa lini kumalizia ujenzi wa hospitali hiyo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, alisema Serikali itamalizia fedha hizo ndani ya muda mchache, lengo likiwa ni wakazi wa Mkoa wa Singida waweze kupata huduma bora za afya.

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, Asharose Matemba (CCM), alihoji Serikali ina mikakati gani ya kuhakikisha watumishi wa sekta ya afya wanakuwa na makazi kwenye maeneo jirani, ikiwa ni pamoja na kuboresha nyumba chache zilizopo na kujenga nyingine mpya.

Akijibu swali hilo, Waziri Jafo alisema Mkoa wa Singida una nyumba 345 za watumishi wa sekta ya afya kati ya 1,072 zinazohitajika, hivyo kuna upungufu wa nyumba 737.

Alisema Serikali inaendelea na ujenzi wa nyumba za watumishi 21 katika vituo vya afya na zahanati na kwamba Sh milioni 280 zimetengwa katika mwaka 2017-2018 kwa ujenzi na ukarabati wa nyumba za watumishi wa sekta ya afya.

“Serikali imeanza kutoa ruzuku ya maendeleo ambayo inatumika kumaliza maboma yaliyoanza kwa nguvu za wananchi katika sekta za afya, elimu na sekta nyingine,” alisema.

Jafo alisema kipaumbele cha matumizi ya fedha hizo kinapangwa na halmashauri zenyewe kupitia mpango wa fursa na vikwazo kwa maendeleo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles