23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 10, 2022

TRA yasitisha minada ya hadhara, sasa kufanyika kielektroniki

Asha Bani, Dar es Salaam

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Edwin Mhede amesitisha kuuza bidhaa balimbali kwenye minada ya hadhara ambayo awali ilikua ikitumia madalali.

Amesema minada hiyo kwa sasa itakuwa kwa njia ya mtandao na kulipiwa kwa njia hiyo licha ya kwamba mteja ataruhusiwa kuona bidhaa alizochagua kwa njia ya mtandao.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa utaratibu uliokuwa ukitumika awali wa minada ya forodha kwa bidhaa mbalimbali ulikuwa ukifanywa kupitia dalali aliyepewa kandarasi  na  TRA kufanya minada hiyo.

“Wakati tulikuwa tukitumia madalali kumejitokeza changamoto mbalimbali ikiwamo kufanyika mara moja kwa wiki na kusababisha bidhaa hizo kutouzwa kwa wakati hivyo serikali kutokomboa kodi kwa wakati pia.

“Pia washiriki wa mnada wamekuwa ni wale wale kwa kujirudia rudia na hata hivyo wengi wao kutokuwa wanunuzi na mara kadhaa kuingilia minada na kuharibu na kufanya wanunuzi wenye nia kushindwa kununua bidhaa hizo,” amesema.

Aidha, amesema kumekuwa na vitendo vya kuzuia wengine na kupanga bei ambayo ni kinyume na busara ya msingi ya uchumi kunakofanywa na baadhi ya watu wenye hila kwa mtandao waliouweka.

Pamoja na mambo mengine, amesema pia tuhuma mbalimbali na vitendo vya rushwa vikihusisha hata baadhi ya Maofisa wa TRA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles