30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 9, 2022

Wana habari watakiwa kusoma ripoti ya CAG

Na CHRISTINA GAULUHANGA

DAR ES SALAAM

WAANDISHI wa habari, wametakiwa kujikita kusoma ripoti mbalimbali na kuandika kwa kina habari’ zinazohusu ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kutoa  elimu kwa umma na kufahamu maendeleo ya taasisi zao mbalimbali.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na mkaguzi kutoka ofisi ya CAG, Lenatus Mnyangabi wakati wa ufunguzi wa warsha kwa waandishi wa habari na namna ya kuripoti taarifa za ofisi hiyo.

Alisema ofisi yao, imekuwa ikitoa hati za aina nne ambazo baada ya kufanya ukaguzi wa hesabu katika idara na taasisi za serikali ambazo ni inayoridhisha, isiyoridhisha, yenye shaka na hali mbaya kulingana na utunzaji nzuri wa hesabu.

Alisema hati za ukaguzi zilizotolewa kwa mwaka wa fedha 2017/18, ulioishia Juni, mwaka jana pia ilifanya kaguzi 255 za Serikali kuu, mashirika ya umma 122, halmashauri 185 na miradi ya maendeleo 469.

“Katika mwaka wa fedha  huo,CAG ametoa hati za ukaguzi 1,031, kati ya hati hizo zinazoridhisha ni 989, zenye shaka 19, zisizoridhisha 17 na hali mbaya sita,”alisema Mnyangabi.

Mkaguzi Mkuu wa Nje,   Alestidia Ngalaba alisema ni vema waandishi wakatumia taaluma yao kuwaelewesha wadau na wananchi kwa ujumla namna ya kusimamia rasilimali na fedha kwa maendeleo.

“Ninaamini kupitia vyombo vyenu, mtatusaidia kuchambua kwa ufasaha kwa kutumia lugha nyepesi ambayo kila mwananchi ataweza kuielewa vizuri na kufanya uamuzi sahihi wa kusimamia matumizi mazuri ya rasilimali za taifa,”alisema.

Alisema uhusiano baina ya ofisi yao na wanahabari,  umesaidia kuleta maendeleo ya nchi kwa sababu kila mmoja amejifunza jinsi ya kutumia na kulinda rasilimali zinazotokana na Kodi.

Ofisa kutoka ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Elias Malima alisema vyombo vya habari, ni mawakala wa umma  na amani, vina kila sababu ya kuisaidia Serikali kutangaza fursa zilizopo na jitihada zinazofanyika.

Alisema wakati huu nchi ikiwa kwenye vita ya kiuchumi, mapambano ya rushwa na kulinda rasilimali ipo haja wananchi nao wakajitokeza kushirikiana na Serikali ili iweze kufikia malengo yake.

“Ni vema ofisi ya CAG, ikawapa fursa wanahabari ya kusoma ripoti zinapotolewa na masuala muhimu ya kuzingatia,”alisema Malima.

Alisema wanahabari wanapaswa kubadilika kwa kuzibeza  taafsiri za kisiasa na kujenga mazoea ya kusoma taarifa za kitaaluma.

Mwishooo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,291FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles