24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

TOSCI yazindua mfumo rasmi wa ukadiliaji wa mahitaji ya mbegu ya mpunga

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Udhibiti na Mbegu Bora Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi amezindua mfumo rasmi wa ukadiliaji wa mahitaji ya mbegu ya mpunga
ambao utarahisisha mawasiliano na kujenga mahusiano bora kati ya wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa mbegu na mamlaka za udhibiti.

Akizumgumza Agosti 29, jijini Dar es Salaam na wataalamu na wadau wa uzalishaji mpunga wakati uzinduzi huo Mkurugenzi wa TOSCI, Ngwediagi amesema mkutano huo ulilenga kupata maendeleo mapya kuhusu zao la mpunga.

Amesema wataalamu wa Tanzania na Kimataifa wameshirikiana kuandaa mfumo huo ili wakulima watumie mbegu bora zilizo thibitiwa na taasisi husika.

“Kuzindua mfumo halisi wa mbegu za mpunga ni wa kisasa ni mara ya kwanza nchini kutumia mfumo huu ikiwa tofauti na huko nyuma utasaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kupunguza gharama,” amesema Ngwediagi.

Aidha, amesema mfumo huo utaonyesha wakulima wanahitaji kiasi gani cha mbegu na kama mahitaji yanaongezeka.

Naye, Mtafiti wa Mifumo ya Mbegu wa Taasisi ya Utafiti wa Mpunga Kimataifa (IRRI), Martin Ndomondo amesema wameweza kufanikisha mahitaji halisi ya mbegu ambapo imekuwa ikichangia wakulima kutopata mbegu za kutosha na wazalishaji kuto kufikisha mbegu moja kwa moja kwa wakulima.

Mtafiti wa Mifumo ya Mbegu wa Taasisi ya Utafiti wa Mpunga Kimataifa(IRRI), Martin Ndomondo.

Amesema kumekuwepo na matatizo baadhi ya makampuni kuzalisha mbegu baada ya mwaka kushindwa kuuzaa na wakulima wakihitaji mbegu lakini hawana taarifa halisi ya kupata mbegu.

“Ujio wa mfumo huu utawawezesha wakulima kuona moja kwa moja kwa urahisi msambazaji gani anapatikana wapi na yupo karibu naye kuweza kufuatilia kupata mbegu kwa kupitia simu janja.

“Utawezesha muuzaji kuingiza kwenye mfumo kiasi gani cha mbegu alichonacho na hivyo kuwezesha ambae ni mdau ni mkulima kumfikia na kuweka oda.

“Mfumo huu umemuunganisha afisa kilimo ambaye yeye anaenda moja kwa moja kwa mkulima na kumuuliza anahitaji Mahitaji gani?,” amesema Ndomondo.

Ameeleza kuwa afisa ugavi atakuwa anapokea mahitaji kutoka kwa wakulima ambao wanahitaji kuagiza kiasi ambacho anaweza kununua kuingizwa kwenye mfumo itakuwa inasajiliwa kutoka ngazi ya kijiji hadi ngazi ya Wilaya.

“Hii itakuwa inasajiliwa kutoka ngazi ya kijiji kwenda ngazi ya kata Afisa ugavi wa kata ataupload kwenye mtandao ambapo itaenda moja kwa moja ngazi ya Wilaya afisa ugavi Wilaya atahakikisha takwimu hizo zitaenda kwa ngazi ya mkoa katika mfumo huo taarifa zinakusanywa ngazi ya Taifa mahitaji ya taifa zima,” ameeleza.

Aidha, amesema mfumo huo utapatikana katika pande mbili utatuma maombi ya simu janja na upande wa tovuti inapatikana kwa sasa ipo kwa simu janja baadaye watawezesha simu zote na kwamba dunia imebadilika wanaenda kidigitali.

Kwa Upande wake Msimamizi Kiongozi wa Afrika wa Mfumo wa Mbegu na Bidhaa wa Taasisi ya Utafiti wa Mpunga Kimataifa (IRRI), Ajay Panchbhai amesema wakulima wanatakiwa kubadilika watumie mbegu bora za mpunga waachana na mbegu za kienyejii au asili.

Amesema Bara la Afrika linatumia gharama nyingi kuagiza chakula nje wakati wana maeneo mazuri ya kuzalisha wakulima bado wanachangamoto ya kuhusu mbegu bora inahitajika elimu zaidi kwa kwakulima ili waweze kuzalisha mpunga bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles