28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Dola milioni 25 kuimarisha mazingira ya Bahari na viumbe hai nchini

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MRADI wa Heshimu Bahari umelenga kuimarisha mazingira ya bahari na viumbe vyake katika maeneo ya hifadhi, ili kukuza hifadhi ya bahari na kuongeza uzalishaji katika rasilimali za baharini na mazalia ya samaki.

Mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) unafanya kazi Tanzania Bara ikiwemo Mkoa wa Tanga, Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam na Mikoa yote ya Unguja na Pemba ambao utagharimu dola za kimarekani milioni 25 hadi kukamilika kwake.

Mkurugenzi Mkaazi wa USAID nchini Tanzania, Craig Hart.

Akizungumza na Wavuvi, wakulima wa mwani na kamati za uvuvi na wanajamii wa Kiijji cha Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja, Mkurugenzi Mkaazi wa USAID nchini Tanzania, Craig Hart alisema wanaunga mkono shughuli zinazofanywa na Rais Samia na Dk. Mwinyi katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Alisema anapenda kuonana na wanajamii ambapo USAID inafanya kazi nao kwa karibu kupitia mradi wa heshimu bahari, kusaidia sekta ya afya,elimu na shughuli zingine za kiuchumi.

Aidha alisema ziara yake hiyo amejifunza mambo mingi ikiwemo changamoto za bahari ikiwemo uvuvi haramu ambapo changamoto hiyo sio kwa Tanzania pekee bali pia katika nchi mbalimbali zilizoendelea hivyo ni vyema kuzibiti hali hiyo na kuwa na uvuvi endelevu ambao kila mmoja kufaidika nao.

Alisema amevutiwa na mandhari ya Zanzibar ambayo yamezungukwa na bahari hivyo yanahitaji kulindwa ili wananchi kuendelea kufaidika na rasilimali zilizomo baharini ikiwemo uvuvi na ukulima wa mwani.

“Mimi napenda sana Samaki na hata Mke wangu anapenda sana mwani hivyo kama hatutoilinda bahari samaki watakosekana lakini pia mwani ni muhimu sana na unafaida nyingi mwilini,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa mradi wa USAID Tanzania Heshimu Bahari, Sadiki Laiser alisema mradi pia umejikita katika kuimarisha sera zitakazosaidia serikali, sekta binafsi pamoja na jamii, kwenye kuimarisha, kuhifadhi, matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.

Alisema mradi huo ni wa muda wa miaka mitano ambapo sasa unaelekea katika utekelezaji wake kwa awamu ya pili ili kuboresha ustawi wa kiikolojia na uzalishaji wa maeneo ya viumbe hai wa baharini nchini Tanzania.

Mratibu huyo, alieleza kuwa mradi huo pia unalengak uwawezesha vijana na wanawake kiuchumi wakiwemo wakulima wa mwani, wafugaji wa majongoo bahari na wavuvi ili kuheshimu kuheshimu bahari na rasiliamli hiyo kuwa endelevu.

Wakizungumza katika mkutano huo, wakulima wa mwani wa kijiji hicho, walisema wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nyenzo zitakazowawezesha kufika katika mashamba yao ya mwani ambapo sasa wanalima katika kina kirefu cha maji ya bahari.

“Hatuna usafiri wa uhakika wa kutufikisha katika mashamba yetu bahari, tunaomba msaada kwa wavuvi watupakie katika boti zao za uvuvi na kutupelekea katika mashamba yetu.wapo ambao baadhi yao wanakubali kutuchukua aidha kwa kulipia au kutupa msaada,” alisema Khadija Juma Ame.

Mkulimam huyo wa mwani alisema wanahitaji nyenzo za kisasa kwa ajili ya kuendeleza kilimo hicho ambacho sasa kinakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa yaliyotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hata hivyo, alisema bado bei ya mwani ni ndogo ambapo kwa kilo moja ni Sh 1,000 hivyo wanahitaji kuongezewa bei kwa sababu kilimo cha mwani kigumu lakini wakulima ambao wengi wao ni wanawake faida wanayoipata ni ndogo ikilinganishwa na wanunuzi wa mwani.

Khadija aliliomba shirika na USAID kusadia masoko ya nje ya zao hilo la mwani ili kuongeza thamani ya mwani ambalo zao hilo ni mkombozi mkubwa wa wananchi hasa wanawake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles