30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

Toeni maoni chanya matumizi ya TEHAMA-Kakele

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Selestin Kakele amesema watu watoe maoni chanya katika matumizi ya TEHAMA ili kuboresha maisha ya Watanzania katika ulimwengu wa kidigitali.

Hayo amebainisha leo Septemba 27, jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu huyo wakati akifungua kikao cha kutoa maoni kuhusu ya sera ya Taifa ya TEHAMA kwa ajili ya makundi Anuai ambapo amesema hichi wanachofanya wataendelea kwa makundi mengine.

Amesema wizara zote zinajukumu la kutunga na kusimamia sera, kanuni, miongozo na sheria ambayo huwa inasimamia utekelezaji wa majukumu wizara wanatekeleza wajibu wa msingi.

“Sera ya TEHAMA ya mwaka 2016 ni mda mrefu umepita na TEHAMA na kama kiumbe ambacho kinazaliwa kinakua na kinabadilika kulingana na wakati na mambo mbalimbali yanatokea duniani katika jamii,” amesema Kakele.

Amesema wakati wanatunga sera hiyo mwaka 2016 hakukuwa na mambo ambayo leo yanatokea hatakama yalikuwepo hakuana mtu angeweza kufasihi miaka michache ambacho kinatokea leo ingekua je?.

Amesema Teknolojia inakua kwa kasi hivyo ipo haja ya kufanya marejeo ya sera ya TEHAMA na kwamba zipo taratibu za kuandaa sera moja ya sharti la msingi ni ushirikwishaji wa jamii.

“Tumekuwa na utaratibu huu tangu tunaanza mchakato wa kukutana na makundi mbalimbali na leo tumeona tukutane na makundi Anuai wenye changamoto mbalimbali za ulemavu lakini ni wadau wetu muhimu katika sera tunajaribu kuifanyia mapitio,” amesema.

Naye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Watu Wenye Ulemavu nchini(SHIVAWATA), Ernest Kimaya amesema sera ya TEHAMA ni muhimu kwa watu wenye ulemavu kutoa maoni kuboresha sera.

Upande wake, Afisa Habari Chama cha Wanawake Wachimba Madini, Halima Mhando amesema hakuna maendeleo yoyote bila mawasiliano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles