24.8 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

DMI yaingia makubaliano na Chuo cha Korea Kusini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaama (DMI), Dk. Tumaini Gurumo amesema chuo hicho  kimeingia makubaliano ya miaka mitano ya kubadilishana uzoefu wa elimu ya Ubaharia na Ujenzi wa Meli na Chuo cha Korea Institute of Maritime and Fisheries Technology ambayo yatawezesha kunufaisha  pande zote mbili za vyuo hivyo kwa walimu na wanafunzi.

Akizungumza mapema Septemba 25, 2023 chuoani hapo, Dk. Gurumo amesema kuwa makubaliano hayo ni muhimu kwa maendeleo ya chuo cha DMI kwa ujumla.

“Chuo cha Korea Istitute of Maritime and Fisheries Technology (KIMFT) kimeendelea kwa Teknolojia ya Ujenzi wa Meli na Elimu ya Ubaharia na wana vifaa vya kisasa hivyo ni muhimu sana kwa chuo cha DMI kupata nafasi hiyo muhimu ya kushirikiana na chuo hicho,” alisema Dk. Gurumo.

Gurumo alisema kuwa makuabaliano hayo yatawezesha wanafunzi wa DMI kwenda chuo cha KIMFT nchini Korea kujifunza elimu ya vitendo ili waendandane na soko la Dunia pamoja na wanafunzi kutoka KIMFT ili kuja kujifunza DMI kuhusu elimu inayotolewa.

Kwa upande wake Balozi wa Korea nchini Tanzania, Kim Yong Jung amesema makubaliano hayo yana manufaa makubwa na yatawezesha wanafunzi wa DMI kwenda nchini Korea kupata mafunzo muhimu ya vitendo katika chuo kikubwa na teknologia ya hali ya juu.

Naye Mwakilishi wa chuo cha KIMFT, Dk. Min Jung amesema kuwa anayofuraha kwa kuingia makubaliano na chuo cha DMI kwani wanafunzi na walimu watapata uzoefu mkubwa katika kuhudumia meli na maswala yote ya ubaharia.

“KIMFT ni chuo cha kwanza kwenye Teknologia na Ujenzi wa Meli katika nchi ya Korea, hivyo naamini chuo cha DMI kitapata uzoefu Mkubwa kwa wanafunzi na walimu kwenda Korea kujifunza,” alisama Dk. Jung.

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Balozi wa Korea nchini Tanzania, viongozi wa chuo cha KIMFT, baadhi ya  wajumbe wa Bodi ya DMI, Uongozi wa Chuo cha DMI na Wanafunzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles