28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Nape awakumbusha watumiaji wa mitandao ya kijamii kulinda usalama

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Habari Mawasilino na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewataka wananchi pamoja na kuwa wanatumia mitandao ya kijamii wahakikishe wanalinda usalama wa jamii na ni muhimu kulinda utamaduni wa Bara la Afrika.

Nape ametoa kauli hiyo leo Septemba 28, jijini Dar es Salaam waziri huyo wakati wa uzinduzi wa mkutano wa Jukwaa la Uhuru wa Mitandao Barani Afrika uliohudhuliwa na wadau mbalimbali kutoka nchi tofauti amesema wameweza kujadili changamoto, faida, fursa na wametoka wapi na wanaenda wapi dunia yote ya mitandao.

Amesema pamoja na nchi kutoa uhuru wananchi wanapaswa kulinda tamaduni kwa kutumia mitandao hiyo katika shughuli za kuwaingizia kipato na si kutumia katika mambo ambayo yanaweza kuvunja amani ya nchi na kuchafua utu wa mtu.

“Tumeweka katika sera zetu uhuru wa mitandao lakini sasahivi dunia imekua, tutumie mitandao hii kufanya shughuli za kiuchumi na si kupiga umbea ambao haukusaidii chochote,” amesema Nape.

Amesema ili kuwa na uhuru mtandaoni nchi za Afrika zinapaswa kulinda tamaduni na ili kuepusha nchi hizo kuingia kwenye matatizo ambayo yatapelekea kuharaibu Amani na kuleta machafuko.

“Tusiondoke kwenye mtandao kila mtu ajiunge huko lakini tuhakikishe tunabaki salama kwa maslahi ya nchi zetu,” amesema.

Aidha, Nape amesema kuwa nchi inajipanga chaguzi zijazo ziweze kutumia teknolojia kwenye uchaguzi ili kumuezesha kila mtu kuchagua viongozi popote atakapokuwa.

“Tunataka ifike mahali kila mwananchi awe na uwezo wa kupiga kura mtandaoni kusiwe na haja ya kwenda kwenye vituo na kupanga foleni kama kila mtu anaweza kutumia simu basi inawezekana ni sisi kuamua kwa kuweka sera nzuri na utekelezaji,”ameongeza.

Amesema zaidi ya watu milioni 34 wapo kwenye mitandao na wanatumia Internet na wanaendelea kuweka mazingira mazuri ya sheria.

Naye Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugakingira amesema kuwepo kwa mkutano huo nchini kumetoka na juhudi zinazofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua nchi kimataifa na kuimalisha uhuru wa habari,uhuru wa kujieleza na haki za binadamu.

“Bara Afrika wakati wa uchaguzi wamekuwa wakizima mitandao inazimwa wakati wa chaguzi zijazo mitandao isizimwe kwa sababu teknolojia imekua itafika mahali watu tutapiga kura mitandaoni,”amesema Lungangira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles