24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TMDA: Mashine inayochuguza viambata hai imeleta msaada Kanda ya Ziwa

Aveline Kitomary, Mwanza

Mchunguzi wa dawa kutoka Mamlaka ya Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi (TMDA) Kanda ya Ziwa, Kapilya Haruni amesema Mshine ya kuchunguza viambata hai imekuwa na msaada mkubwa katika eneo hilo la Kanda ya Ziwa.

Haruni anasema, maabara hiyo inamashine ya kisasa ambayo inaweza kuchunguza uwezo wa dawa katika mwili wa binadamu.

Akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika maabara hiyo iliyopo jijini Mwanza, Haruni amesema mashine hiyo inayoitwa ‘desolution tester machine’ imekuwa msaada mkubwa katika eneo hilo la kanda ya Ziwa katika kuchunguza viambata hai vya dawa mbalimbali.

“Mashine hii kazi yake ni kuangalia namna gani dawa inaweza kuachia kiambata hai ambacho kipo ndani yake kwa kiwango kinachotakiwa ili iweze kuingia katika mwili wa binadamu na kufanya kazi kwa kiwango kilichokusudiwa.

“Mashine hii pia inaweza kutumika katika maeneo mbalimbali ya utengenezaji wa dawa kwa maana kwamba dawa inapotengenezwa inakuwa na viambata vingine ambavyo sio hai, hivyo mtengenezaji ili kujiridisha kwamba dawa aliyotengenezwa kiambata hai iliyopo itatoka kwa kiwango kinachotakiwa atatumia mashine hii,”amefafanua Haruni.

Mchunguzi wa dawa Kapilya Haruni akionesha jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi kama tumbo la mwanadamu

Ameeleza kuwa wanapotaka kupima kiambata hai wanalinganisha na mwongozo wa kimataifa wa dawa husika hivyo mashine hiyo inauwezo mkubwa kutambua dawa.

“Mtengenezaji wa dawa ni vizuri akafanya ulinganishwaji na mwongozo wa dawa husika ambao umeandaliwa (reference madicine) au dawa ya kufanyia mlinganisho.

“Kiwango cha kiambata hai inaweza kupimwa na mashine hii ambayo itaachanisha kiambata hai na kile ambacho sio hai na katika hatua hiyo tunaweza kutumia mashine zingine maalum kupima kiwango,” amesema.

Amesema upimaji kutumia mashine hiyo ni rahisi kutokana na kuwa na mfumo wa moja kwa moja (automatic) na kutoa kiwango kinachotakiwa kwa muda maalum.

“Kiambata hai ni ile kemikali ambayo inatambulika kisayansi kuwa inaleta tiba katika mwili wa binadamu kutokana na tafiti hizi kemikali zinaweza kuleta madhara hasi au chanya na endapo kiwango kitazidi inaleta madhara.

“Mashine hii inafanya kazi mithili ya tumbo la mwanadamu unaweka kwa muda ulio’set’ kama dakika 15 ili dawa iweze kuyeyuka hivyo ina’test’ myeyuko wa dawa na isipokuwa imeyeyuka haiwezi kufanya kazi iliyokusudiwa.

“Kwani dawa inapotumiwa na kuyenyuka inavunjika katika vipande ndipo inaweza kuingia kwenye seli kufanya kazi yake kama itabaki ilivyo haitafanya kazi iliyokusudiwa.

“Ndani ya hii mashine kuna vifaa tunaweka vimiminika ambavyo ni sawa na vile vilivyoko tumboni kwahiyo kama mwongozo utasema dawa hii inayeyuka kwenye asidi iliyoko tumboni ( hydcloric acid) flani basi kiwango hicho na sisi tunatengeneza na kuweka katika vibebeo vilivyopo katika hivi Vifaa,” anasema.

Aidha, anabainisha kuwa kitu kingine wanachoangalia ni kiwango cha joto cha mwili wa mwanadamu ambacho kinatakiwa kufanana na mashine hiyo kuanzia nyuzi 36 hadi 37 ili kuweka mazingira sawa na tumbo.

“Baada ya hapo tunachukua vimimika maalum vilivyotolewa mashine hii inafanya myeyuso halafu tunaenda kwenye mashine nyingine
tunaweka muda kama itayeyuka kabla ya muda unaotakiwa kulingana na mwongozo inawezekana haijatengnezwa vizuri na ikichukua muda mrefu pia kutakuwa na tatizo katika utengenezaji.

“Baada ya hapo tunaenda kwenye mashine ambayo inaonesha kiambata kilichopo katika dawa hii ni kiasi gani na pia tutaweka kwenye mashine nyingine ambayo itasoma katika intesty ya dawa husika,”amefafanua Haruni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles