24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Timu 17 zathibitisha Klabu Bingwa Netiboli

Anna Kibira
Anna Kibira

NA ASMA BASHIR, DAR ES SALAAM (DSJ)

TIMU 17 zimethibitisha kushiriki mashindano ya Klabu Bingwa ya Netiboli yaliyopangwa kufanyika Julai 12 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli nchini (CHANETA), Anna Kibira, alisema timu hizo zimethibitisha kushiriki mashindano hayo huku timu tatu za Filbert Bayi ambao ndio mabingwa watetezi, Teachers ya Kinondoni na Polisi ya Mbeya wakijiondoa.

Alizitaja timu zitakazoshiriki kuwa ni Jeshi Stars, JKT Mbweni, Polisi, Uhamiaji, CMTU zote kutoka Dar es Salaam.

Nyingine ni JKT Ruvu, TTPL ya Morogoro, Polisi Dodoma, Magereza Morogoro, Polisi Shinyanga, Polisi Mwanza, Polisi Kigoma, Mbeya City Queens, CIDT Arusha, Polisi Arusha, Nyanyembe ya Tabora na Polisi Morogoro.

Timu zitakazoshika nafasi ya kwanza hadi ya nne zitashiriki Ligi ya Muungano itakayoanza Agosti mwaka huu.

“Tutatumia mashindano hayo kuteua wachezaji wenye nidhamu na uzalendo watakaoungana na wenzao wa Zanzibar kuunda timu yetu ya Taifa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles