26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

TIKETI ZA MABASI KUKATWA KWA A SIMU

Na Mwandishi Wetu

-Dar es Salaam

NI wazi sasa  siku za wapiga debe katika vikuto vikubwa vya mabasi nchini zinaanza kuhesabika.

Hiyo ni baada ya Serikali kwa kushirikiana na wamiliki  wa mabasi, kujiandaa kutumia mfumo mpya wa ukataji wa tiketi kwa njia ya elektroniki na siku za kiganjani.

Hatua hiyo  imekuja baada ya wamiliki wa mabasi kukubaliana kwa kauli moja  kuwa mfumo mpya  ambao sasa uko hatua za mwisho katika makubaliano na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kabla ya kutumika, utaisidia kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikipotelea mikono mwa wapiga debe.

“Tunaamini ukataji wa teketi kwa njia hii utasaidia  kuingiza mapato serikalini, lakini pia kwa wamiliki ambao wamekuwa wakipoteza fedha nyingi kwa mawakala au wapiga debe,”alisema mmoja wa wamiliki wa mabasi hayo.

Akizungumza na MTANZANIA  Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa Kampuni ya E-Ticketing Systems  (ETS), Martin Kaswahili, alisema lengo la kutumia mashine za EFD ni kuingizia mapato ambayo yatakwenda moja kwa moja kwa wamiliki na serikalini.

Alisema mfumo huo, ni wa kisasa kwa sababu  umekuwa ukutumika nchi nyingi duniani.

“Mmliki anaunganishwa moja kwa moja na mfumo wa kodi, abiria akikata tiketi kwa njia ya simu taarifa zake zitaifikia TRA moja kwa moja, huku mmiliki akipata fedha zake bila kupoteza hata senti,”alisema.

Alisema tayari jambo hilo limejadiliwa kwa kina katika vikao kati ya maofisa wa TRA na wamiliki wa  mabasi, huki pande ikiafikia kuwapo mfumo huo.

  Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA),  Enea Mrutu  aliliambia gazeti hili jana  mfumo huo mzuri utaokoa fedha nyingi zilizokuwa zikipotea.

“Mfumo huu nakubaliano nao, naamini umekuja wakati mzuri mno, wamiliki tumekuwa tukipoteza fedha nyingi kwa wapiga debe nchi nzima…hili ni jambo jema  tunapaswa kuungana wote,”alisema Mrutu.

Alisema tayari wamekutana na Kamishna wa Kodi  kutoka TRA, Udani Mwambusi na viongozi wengine wa mamlaka hiyo   kujadili jambo hilo kwa kina.

Alisema katika kikao hicho,  walijadili mambo mbalimbali ikiwamo jinsi TRA itakavyoweza kupata kodi kupitia mfumo wa EFD moja kwa moja.

Alisema walikubaliana mambo matatu ya kufanya  ikiwa ni pamoja na marekebisho juu ya kulipwa asilimia mbili juu ya mtandao huo, kukusanya fedha  na mkataba wa muda mrefu ambao awali ulikuwa ni wa miaka mitano, huku wamiliki wakitaka uwe wa muda mrefu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles