29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

KAMPENI YA KUWALINDA WATOTO YAANZA DAR

Na ASHA BANI

-DAR ES SALAAM

SERIKALI kwa kushirikiana na taasisi za  jamii nchini imezindua kampeni  ya kuwalinda watoto inayotambulika kwa jina la ‘Thamani ya mtoto ni maisha leo na kesho’ itakayoendeshwa kwa   miaka mitano.

Mratibu wa Kampeni hiyo, Janeth Mwasawala alisema kampeni hiyo itashirikisha mashirika mbalimbali yanayowahusu wanawake na watoto kwa kuona ni jinsi gani ya kumsaidia mtoto.

Alizitaja taasisi  zilizounganisha nguvu ya pamoja katika kampeni hiyo kuwa ni  a Women In Society, Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), UDSM Female Students Association, Women Fund Tanzania, Purple Planet, Eve Enterprises Co.Ltd, TCRS na ECAW.

Alisema mtoto ni tunu ya taifa na kwa kushirikiana na kamati hiyo watahakikisha mtoto anathaminiwa leo na kesho.

“Ili kujenga maisha yake ya kesho lazima mtoto athaminiwe na jamii nzima, leo ukimthamini mtoto na kesho ukimthamini motto, yeye mwenyewe ataona thamani yake.

“Ni lazima tupinge ukatili kwa watoto ambao unaendelea siku hadi siku na kuona ni nini kitapunguza ukatili huo ambao ni pamoja na usalama barabarani, shuleni, nyumbani na eneo lolote atakalokuwa katika maisha yake ya kila siku,’’ alisema Mwasawali.

  Ofisa Ustawili wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue, alisema  kampeni hiyo ni muhimu na   itasaidia kupinga  vitendo vingi vya ukatili zikiwamo  mimba za utotoni na unyanysaji ikizingatiwa takwimu zinazidi kuongezeka.

“Kampeni hii iende sambamba na  usalama barabarani, viboko kwa watoto na kwa pamoja tukimthamini motto takwimu ya unyanyasaji kwa watoto itapungua kwa sababu  sasa unyanyasaji umekuwa mkubwa tofauti na miaka iliyopita na hii inatokana na u ‘busy’ kwa wazazi na walezi.

“Tukishirikiana na watu mbalimbali katika kampeni hii  kama jamii, shuleni na majumbani hasa matukio ya ubakaji ambayo yamekuwa yakijitokeza siku hadi siku yatapungua kwa sehemu kubwa,”alisema Masue

Alisema kuna umuhimu wa kuwatunza na kuwajali watoto  kwa vile  jukumu la kuwasimamia na kuwatunza ni la wote katika jamii.

Alisema miongoni mwa mambo ambayo mtoto anapaswa kuyapata ni pamoja na chakula chenye lishe bora,tangu akiwa tumboni kwa mama yake na kuvaa vizuri ajue na yeye kuwa anathminiwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles