25.6 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

TEKNO ACHUKIZA MASHABIKI KENYA

NAIROBI, KENYA


MASHABIKI wa muziki nchini Kenya, wametumia mitandao ya kijamii kuiponda shoo ya mkali kutoka nchini Nigeria, Tekno Miles, iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Nairobi.

Msanii huyo alikuwa nchini humo kwa ajili ya tamasha la The Wave Concert, lakini shoo yake ilionekana kuzomewa na mashabiki wengi kutokana na vyombo kutosikika wakati vikipigwa ‘Live’.

Msanii huyo alitumia dakika 28 jukwaani, lakini hakuweza kuwafurahisha mashabiki ambao walijitokeza kutokana na wapiga bendi wake kushindwa kuseti vizuri vifaa vyao.

Hata hivyo, DJ maarufu nchini humo, Creme De La Creme, alitumia ukurasa wa Twitter kuwaambia mashabiki kwamba, Tekno alikuja kwenye shoo hiyo bila ya kujiandaa na si tatizo la vyombo kama watu wanavyosema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,504FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles