33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

GABO: KUENDEKEZA BIFU NI KUJIMALIZA

NA JESSCA NANGAWE-DAR ES SALAAM


MKALI wa Filamu za Bongo, Gabo Zigamba, amesema wasanii kuendekeza bifu  ni dalili za kujimaliza kabisa na kukosa ubunifu kwenye kazi zao.

Hivi karibuni msanii huyo amejikuta katika ugomvi na msanii mwenzake, Daudi Michael maarufu kama Duma kutokana na kila mmoja kumlalamikia mwenzie kushindwa kuitendea haki tasnia hiyo.

Gabo amesema kuendelea kuzozana na Duma ni kujidhalilisha, kwani kufanya hivyo ni kujimaliza zaidi katika kazi zao.

“Unadhani bifu kama hizi zinasaidia? nadhani ni kuendelea kujichimbia kaburi na kupotea kabisa katika ramani ya sanaa, tushindane katika kutoa kazi nzuri, zenye ubunifu  kwa masilahi yetu na ya mashabiki,” alisema Gabo.

Gabo amekuwa akilalamikiwa na Duma  kuwa ni mmoja wa wasanii ambao wanadidimiza tasnia ya filamu kutokana na kupewa hadhi kubwa ambayo kwa sasa inaonekana kumzidia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles